Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe, amezungumzia jinsi ambavyo uboreshawaji wa huduma za mawasiliano zinavyochochea kubadili maisha ya watu kupitia kuboreka kwa shughuli za kiuchumi na kijamii huku akipongeza maamuzi ya kampuni ya Vodacom ya kupelekea mawasiliano kwenye kisiwa cha Goziba kilichopo Ziwa Viktoria eneo la mkoa wa Kagera.
Kanali Masawe, ameyasema hayo wakati alipotembelea Makao Makuu ya Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom jijini Dar es salaam na kukutana na Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wake Georgia Mutagahywa ikiwa ni sehemu ya kutoa Shukurani kwa kufanikisha kuweka mnara wa simu katika kisiwa cha Goziba pamoja na kusaidia ujenzi wa kituo cha afya kisiwani humo kupitia Vodacom Foundation.
Amesema tangu Goziba ilipounganishwa kwenye mtandao wa simu za mkononi kumekuwepo na mabadiliko makubwa katika maisha ya wakazi wa kisiwa hicho huku ikisaidiwa kwa kiwango kikubwa suala la ulinzi na usalama na kuifungua Goziba.
“Tunawashukuru sana Vodacom, mmekuwa wa kwanza kufikisha huduma za mawasiliano ya simu kisiwani Goziba na hivyo kuwafanya wakazi wake kuendelea kuwakumbuka kwa namna mlivyowakomboa. “Alisema Massawe.
“Hali ya ulinzi na usalama kwenye kisiwa cha Goziba haikuwa nzuri hata kidogo, kisiwa kilikuwa kikibaliwa na wimbi kubwa la uvamizi wa majambazi waliokuwa wakiwavamia wavuvi na kuwapora fedha na mali zao ikiwemo nyavu na mashine za boti huku wakikosa msaaada wowote kwani kisiwa hakina kituo cha Polisi na hawkauwa na namna ya kuomba msaada kutoka Bukoba kutokana na kukosa huduma za mawasiliano.”
Pamoja na kuipongeza kampuni hiyo, Kanali Masawe amesema kuwa, huduma hizo za Mawasiliano pia zimefungua fursa za kiuchumi kwa wakazi wa kisiwa hicho ambacho sasa wanawasiliana moja kwa moja na watu walioko katika maeneo mengine ya nchi na hata nje ya Nchi hususa Nchi jirani ya Kongo ambayo wanafanya nayo biashara ya kuuza dagaa.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fabian Massawe akihojiwa na Mhina Shemweta wa kampuni ya Gin Din inayotoa huduma za ushauri wa masuala ya Mawasiliano kwa kampuni ya Vodacom Tanzania. Katikati ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim. Kanali Massawe alifika Makao Makuu ya Vodacom jijini Dar es salaam kwa shughuli za kikazi
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fabian Massawe akifurahia jambo na Mfanyakazi wa Vodacom Shomary Shomary mara baada ya kukumbushana enzi za Kanali Massawe alipokuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee wakati huo Shomary nae akiwa ni mwanafunzi shuleni hapo. Wawili hao walikutana wakati Mkuu huyo wa Mkoa alipofika Makao Makuu ya Vodacom kwa shughuli za Kikazi.Kanali Massawe ni mmoja
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fabian Massawe (wa tatu kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Muleba Lembris Kipuyo (wa pili kushoto) wakiwa pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom ambao baadhi yao walifundishwa na Kanali Massawe wakati alipokuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee jijini Dar es salaam.Kanali Massawe alifika Makao Makuu ya Vodacom kwa shughuli za kikazi ambapo alivuta hisia za wafanyakazi waliowahi na hata ambao hawakuwahi kupitia mikononi mwake enzi za ualimu na hivyo kuleta hali ya furaha ikitawaliwa na utani na ukumbusho wa matuko ya Shule.
Asante VODACOM,Bado maeneo ya vitongoji vya kyaka ukishapita kyaka, bunazi, kasambya,ukiendelea mbele ndio basi hupatikani kabisaaa.
ReplyDelete