Mwenyekiti wa Baraza, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, akitoa hotuba ya utangulizi kabla ya Mkuu wa mkoa wa Pwani, B. Mwantumu Mahiza hajafungua rasmi Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Uchukuzi, lililofanyika mjini Bagamoyo katika hoteli ya Millenium Beach Resort, leo asubuhi.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bi. Mwantumu Mahiza akitoa hotuba wakati akifungua Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Uchukuzi, lililofanyika mjini Bagamoyo, leo asubuhi katika Hoteli ya Millenium Beach Resort.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bi. Mwantumu Mahiza (wa nne kutoka kulia waliokaa), akiwa katika picha ya Pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Uchukuzi, mara baada ya kulifungua katika Hotel ya MIllenium Beach Resort, mjini Bagamoyo, leo asubuhi. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-UCHUKUZI).

Juhudi za Seriali za kuboresha sekta ya Uchukuzi hazitachangia ipasavyo katika kuinua uchumi wa Taifa endapo watumishi  wa Serikali hawatabadilika na kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa Mazoea.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mwantumu Mahiza amesema hayo leo katika ufunguzi wa Baraza la Wafanayakazi la Wizara ya Uchukuzi mjini Bagamoyo.

Mhe Mahiza amesema kila mtumishi katika eneo lake la kazi anapaswa kufanya kazi kwa kujituma, weledi na kwa ubunifu ili kuboresha mchango wa wizara ya uchukuzi katika kuboresha na kukuza uchumi wa Taifa la Tanzania.

Amesema Wizara ya Uchukuzi ni Sekta nyeti katika maisha ya kila siku katika uendelezaji wa shuguli za kiuchumi na kijamii, hivyo wadau katika sekta hii wanapaswa kushiriki na kushikamana katika utendaji wa kazi hiyo.

‘Utekelezaji wa majukumu ya kazi kila mdau anatakiwa ajiulize yeye mwenyewe katika sehemu yake amechangia nini au ameleta mabadiliko gani katika sekta ya usafirishaji na uchukuzi. Ili kuleta mabadiliko katika sehemu ya kazi. Wadau katika sekta ya Uchukuzi wanapaswa kuachana na kufanya kazi kwa mazoea na kufanya kazi kwa ubunifu na kujituma kwa kiwango cha juu’. Alisema Mhe. Mahiza.

Ili watumishi waweze kufanya kazi kwa matokeo makubwa, Mhe. Mahiza ameshauri Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Dkt.  Shaaban Mwinjaka kuwapa motisha kwa kuwapandisha vyeo na kuwasomesha na kuwapa fursa za kutembelea hifadhi za mbuga za wanayama ili kuwahamasisha na kuwaongezea mori na ari ya kufanya kazi.

Akizungumzia changamoto ambazo wizara ya Uchukuzi inakabilian nazo, Mkurugenzi Msaidizi, Usimamizi wa Rasilimali watu, Bi. Judith Ndaba amezitaja changamoto hizo ni pamoja na uhaba wa watumishi katika Wizara.

‘Wizara inajitahidi kukabiliana na changamoto hiyo kwa kuhakikisha kuwa kila sehemu iliyo wazi imejazwa watumishi. Tayari Wizara imeomba kibali kuitaka Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma kwa lengo la kujaza nafasi hizo ili kuchangia ipasavyo katika utekelezaji wa mpango wa matokeo makubwa sasa(BRN)’.Alisema Bi Ndaba.


Mkutano wa Baraza la wafanyakazi la wizara ya uchukuzi,ambao umefanya kwa siku moja,ulipitia utekelezaji wa mpango mkakati wa mwaka 2013/14 na kupitisha mpango mkakati wa mwaka 2014/15.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...