Watanzania waishio nchini Malaysia hivi karibuni walikutana pamoja katika hafla ya kusherehekea maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanzania zilizofanyika katika Hotel ya Prince jijini Kuala Lumpur- Malaysia,chini ya uongozi wa Balozi Dr. Aziz Ponary Mlima. Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo alikuwa ni Naibu Waziri wa Usafiri na Uchukuzi wa Malaysia Dato Ab. Aziz Kaprawi.
Balozi wa Tanzania nchini Malaysia,Dr. Aziz Ponary Mlima pamoja na Maafisa wa Ubalozi wakiwakaribisha wageni waalikwa.

Picha ya waliokaa, katikati ni mgeni rasmi ambaye ni Naibu Waziri wa Usafiri na Uchukuzi wa Malaysia Dato Ab. Aziz Kaprawi, kulia kwake ni Balozi Abdul Samad bin Othman ambaye ni Mkurugenzi wa Afrika katika wizara ya mambo ya nje ya Malaysia na kushoto kwake ni Dr. Aziz Ponary Mlima, Balozi wa Tanzania Malaysia.
Balozi wa Tanzania nchini Malaysia,Dr. Aziz Ponary Mlima (kulia) pamoja na mgeni rasmi ambaye ni Naibu Waziri wa Usafiri na Uchukuzi wa Malaysia Dato Ab. Aziz Kaprawi wakikata keki kwenye hafla hiyo ya kusherehekea maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanzania zilizofanyika jijini Kuala Lumpur- Malaysia.
Sehemu ya watanzania waishio nchini Malaysia wakiwa pamoja na wageni wao katika hafla hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...