Na Richard Bagolele Chato

Mradi wa kuhifadhi mazingira ya  ziwa Victoria awamu ya pili (LVEMP II) Wilayani Chato unategemewa kuboresha ubora wa Dagaa na Furu katika mialo mbalimbali Wilayani hapa.

Mradi huo ambao unasimamia na kuhifadhi mazingira ya ziwa Victoria umeanza kwa kuunda kamati mbalimbali wilayani hapa ambazozinasimamia udhibiti wa Gugumaji, kuhifadhi na kulinda mazalia ya samaki na mradi wa kituo cha kuzalisha wadudu aina ya  Mbawakavu  ambao hushambulia mmea wa Gugumaji.

Mratibu wa mradi huo wilayani Chato Bw. Salvatory Mutajukwa amesema katika kuhakikisha mradi wa uhifadhi wa mazingira ya ziwa Victoria unakuwa endelevu  kamati husika  zimeanzisha miradi ya kipato ili kufanya zoezi hilo kuwa endelevu. 
Ameitaja baadhi ya miradi hiyo iliyoibuliwa na kamati ni pamoja na ufugaji wa kuku wa asili,ufugaji wa samaki kwenye mabwawa, mradi wa kuchakata dagaa na furu. 

Mwalo wa Chato Beach mradi wa LVEMP II kuna kituo cha kuzalisha mbawakavu na mradi wa kipato ni kuchakata Dagaa na Furu ili kuwezesha Dagaa na Furu wanaovuliwa ziwa Victoria kukaushwa na kuhifadhiwa katika mazingira safi na salama. 

Katika mwalo wa Kahumo kata ya Muungano kuna mradi wa kuhifadhi kondo la mazalia ya samaki na udhibiti wa gugumaji, wanajamii chini ya kamati ya usimamizi wameibua mradi wa ufugaji kuku kama mradi mbadala wa kujiongezea kipato. 

Katika Mwalo wa Mlila kamati ya usimamizi wa mazingira ya ziwa Victoria  unaojihusisha na kuhifadhi wa mazalia ya samaki na kuopoa gugumaji umeanzisha mradi wa ufugaji kuku wa asili kama njia mojawapo ya kuongeza kipato cha kamati inayosimamia mradi.

Mwenyekiti wa kamati ya kusimai mradi Mlila Bw. Matete Simba amesema baadhi ya changamoto zinazowakabili katika zoezi zima la uhifadhi wa  mazingira ya ziwa Victoria ni pamoja na Jamii kuendeleza kilimo kandokando ya ziwa kitendo kinachokwamisha suala zima uhifadhi wa ziwa Victoria.

Timu ya menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Chato iliyotembelea miradi hiyo  tarehe 16 Aprili 2014 na kujionea shughuli zinazofanywa na wanakamati husika imezishauri kamati husika kutumia fedha hizo kwa uwazi na kuhakikisha thamani ya pesa kwenye miradi inaonekana.
Mwonekano wa Mwalo wa Nyamirembe uliopo Chato.
Mratibu wa LVEMP (W) Chato Bw. Salvatory Mtajukwa (wa tatu kutoka kushoto)akielezea juu ya mradi wa ufugaji wa kuku wa asli mwalo wa Mlila.
Jengo la mradi wa LVEMP lililoko mwalo wa Chato Beach kwa ajili ya mradi wa kuchakata Furu na Dagaa.
Banda la kufugia kuku wa asili lililopo Mwalo wa Mlila.
Afisa habari wa Halmshauri ya Wilaya ya Chato Bw. Richard Bagolele (kushoto) na afisa Maendeleo ya Jamii (W) Bw. Dionis Mtayoba (katikati) pamoja na mwenyekiti wa kijiji cha Nyamirembe (kulia) wakiwa kwenye mtumbwi uliotolewa na LVEMP kwa ajili ya kuendeshea shughuli mbalimbali za uhifadhi wa ziwa Victoria.
Baadhi ya wakuu wa idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato ) wakiwa kwenye mtumbwi uliotolewa na LVEMP kwa ajili ya kuendeshea shughuli mbalimbali za uhifadhi wa ziwa Victoria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tumieni Life Jacket musije kuilaumu Serikali.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...