Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi la Tanzania wamefanikisha kuifungua barabara ya Kongowe kuelekea Mjimwema hadi Kigamboni ambayo ilijifunga kutokana na kukatika kwa kalvati katika mto Mtokozi . Kalvati hilo lilibomolewa na mvua kubwa zilizonyesha kwa siku kadhaa hapa jijini.

Hapo jana siku ya Jumanne, Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pia alishirikiana na watendaji kwa siku nzima akiwa eneo la Mpiji kuhakikisha barabara ya Dar es Salaam kuelekea Bagamoyo inaanza kupitika tena baada ya kuwa imejifunga kwa takriban siku tatu. Sehemu hii ya barabara iliathiriwa na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha katika kipindi cha hivi karibuni. Matengenezo katika daraja la Mpiji yalikamilika jana usiku na magari yameanza kupiti bila ya matatizo.

Siku ya Jumatatu daraja jingine katika katika mto Kizinga kwenye barabara ya Kilwa eneo la Mbagala Kongowe ilifunguka baada ya kazi ya usiku kucha iliyoongwozwa na Waziri Magufuli kufanikisha kukamilisha matengenezo katika sehemu hiyo yenye magari mengi. Barabara ya Kilwa ndiyo kiungo kikuu cha usafiri wa barabara kati ya Dar es Salaam na mikoa ya kusini.

Aidha katika siku hiyo hiyo ya Jumatatu, daraja la Ruvu pia lilianza kupitisha bagari baada ya sehemu ya barabara iliyokuwa imeharibika kutokana na mafuriko, kukarabatiwa.
Matengenezo yakiendelea katika Daraja la Mpiji.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akifuatilia matengenezo katika Daraja la Mpiji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hongera sana kwa kazi nzuri ya kurejesha hii barabara. Lakini natoa mapendekezo, sijui tu kama ni mimi ninayeona hizi picha yaani, raia wakiwa karibu na eneo la kazi, kuna ajali nyingi tu ambazo zinaweza kutokea hapa, Tipa inamwaga mawe harafu tunaanza kusema mapenzi ya mungu, jamani tuondoe matatizo mengine...

    ReplyDelete
  2. Fanya kazi baba, tupo nyuma yako achana na thamthilia za Dodoma.

    ReplyDelete
  3. Tunataka Waziri jembe kama Magufuli.

    Yupo on site everywhere!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...