Sehemu ya njia ya reli katika eneo la Ming’ongo ikiwa inaning’inia baada ya tuta
kusombwa na maji kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali
nchini Tanzania. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Kipalo Amani
Kisamfu pamoja na wakurugenzi kutoka Wizara ya Uchukuzi wametembelea eneo hilo leo
mchana kuona athari kubwa iliyotokea kwenye njia ya reli. Aidha, katika njia hiyo kilomita kumi
na nane za njia ya reli zimeaharibiwa na mvua hizo zinazoendelea kunyesha katika mikoa
mbalimbali nchini Tanzania.
Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Reli, Wizara ya Uchukuzi, Bw. Festo
Mwanjika (wa pili kutoka kulia) akiangalia uharibifu mkubwa uliotokea kwenye njia ya reli katika
eneo la Ming’ong’o kilomita 4 kutoka Stesheni ya Ruvu, alipotembelea eneo hilo kujionea moja
kati ya sehemu kumi na nane zilizoharibiwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Uchukuzi)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...