Mwanamuziki mwashuhuri wa Reggae Afrika mashariki Jhikoman kutoka Bagamoyo Tanzania,anatarajiwa kuondoka nchini katikati ya mwezi huu April 2014 kuanza ziara ya miezi mitatu barani ulaya,ambapo atatumbuiza katika maonyesho makubwa ya kimataifa huko ughaibuni.
Baadhi ya festival zitakazo funikwa na mwanamuziki huyo ni Helsink Film Festival kule Finland, na Norway na imebainika kuwa Jhikoman pia atashea uwanza moja wa gwaride na wazee wa kazi FFU Ughaibuni aka "watoto wa mbwa" Ngoma Africa band katika maonyesho makubwa ya Tubingen,Ujerumani yatakayo fanyika kuanzia 17 mpaka 20 Julai 2014.
Habari zimetonya kuwa Jhikoman & Afrikabisa Band ametajwa kuwa ni balozi nyota bora ya Reggae anayekubalika kimataifa na anaweza kumudu kutingisha jukwaa lolote kubwa la kimataifa.
usikose at http://www.jhikoman.com
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...