Na Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu nane kwa makosa mbalimbali ya uhalifu kufuatia msako uliofanyika tarehe 01/04/2014 maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME - SACP amesema tukio la kwanza alikamatwa SIMON S/O MTUNDU, miaka 51, Kabila Mhehe, mkulima na mkazi wa kijiji cha Kisisi Kata ya Kimagiyi Tarafa na Wilaya ya Mpwapwa, akimiliki silaha aina ya Gobore lenye Namba MP. 00202182 kinyume cha sheria za umiliki wa silaha.

Kamanda MISIME amesema tukio jingine alikamatwa CHISEMI S/O ROBERT, miaka 34, kabila Mgogo, mkazi wa kijiji cha Kiboriani Wilaya ya Mpwapwa na wenzake wawili wakimiliki shamba la bhangi ekari moja na nusu (1.5) kinyume cha sheria. Shamba hilo limefyekwa na kuteketezwa kwa moto.

Aidha katika Wilaya ya Chemba Mkoani humo alikamatwa MUSSA S/O ALLY MADEBE, mwenye miaka 20, mkulima wa Kijiji na Kata ya Songolo Tarafa ya Goima na wenzake watatu wakiwa na misokoto nane ya Bhangi,  watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara upelelezi utakapokamilika na msako bado unaendelea.

Kamanda MISIME amewashukuru wananchi hawa wanaoshirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa na kushirikiana na Polisi katika misako.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...