Mke wa Makamu wa RaisMama Asha Bilal  (L)na Mlezi wa chama cha wake wa viongozi Mama Tunu Pinda wakipata maelezo kutoka kwa Prof Amyn Alidina ambaye ni mkuu wa kitengo kinachotoa   huduma ya matibabu ya ugonjwa wa Saratani inayo tolewa katika Hospitali ya Aga Khan iliyopo jijini Dar es salaam Wake wa viongozi walikuwa katika Hospitali ya Aga Khan katika kampeni ya kuhamasisha Watanzania kuwa natabia ya kuchunguza afya zao ilikujua mapema kama wanatatizo la Saratani  nawaweze kupata matibu matibabu yanyo stahili Picha na Chris Mfinanga
 Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal (R) akiwa na mlezi wa chama cha Wake wa Viongozi Mama Tunu Pinda (C)wakipata maelezo kutoka kwa Dr Sittileila Twaha  kuhusu saratani aliyokuwa nayo  mgonjwa Rehema Hatibu (53) ambaye anapata matibu Wake wa viongozi walikuwa katika Hospitali ya Aga Khan katika kampeni ya kuhamasisha Watanzania kuwa natabia ya kuchunguza afya zao ilikujua mapema kama wanatatizo la Saratani nawaweze kupata matibabu yanyo stahili Picha na Chris Mfinanga. 

Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda akipokea zawadi ya uwa kutoka kwa Loveluck Mwasha ambaye ni  Muuguzi mkuu wa Hospitali ya Aga Khan kama ishara ya shukurani  katika kampeni ya ugonjwa wa saratani

======  =======  =======

 Kikundi cha wake wa Viongozi (New Mellinium Women Group) kimetembelea Hospitali ya Aghakan  jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya Kampeni Maalumu ya Uhamasishaji wa K ampeni ya Saratani ya Matiti iliyoanzishwa na Hospitali hiyo.


Kwa niaba ya wake wa Viongozi Mlezi wa chama hicho cha wake waviongozi ambaye ni Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda amesema , “Wake wa viongozi wameguswa na kuona kuwa wao ni mabalozi wa wakinamama kwa njia moja ama nyingine wanaweza  kutoa elimu kwa ndugu jamaa na jamii iliyowazunguka katika kutoa uhamasishaji wa Kampeni ya Saratani”.

Mama Pinda ,amesema ni vema wakinamama kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara kwani matibabu ya Saratani yanatibika hivyo kuwahi kupata vipimo na kugundua tatizo mapema itaweza kuponya kinamama wengi hapa nchini ambao hupoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.

“Kansa haina umri, kuna kinga kuanzia kwa watoto wenye umri chini ya miaka 12 hivyo nawasihi wakina mama kutumia nafasi waliyopewa kwenda kufanya vipimo vya Saratani vilivyoanzishwa katika Hospitali ya Agakhan”, alisisitiza Mama Pinda.

Mama Gharib Bilali alisema, “miongoni mwa saratani inayosumbua kina mama ni saratani ya Shingo ya Uzazi, natoa wito kwa watanzania hasa kina mama kwenda kufanya vipimo vya Saratani hiyo ili kuweza kujua afya zao kwani mama ni sehemu muhimu sana katika familia nawasihi wakinamama kutumia nafasi hii adhimu iliyotolewa na Hospital ya Agakhan kwenye kufanya vipimo hivyo”.

Mapema Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Aga khan Bibi. Loveluck Mwasha alisema, ujio wa wake wa Viongozi (New Millenium Women Group) imeamsha ari na kutupa moyo na kuona ni jinsi gani wake hao wameguswa na jambo hili muhimu kwani wao ni mabalozi ambao wataweza kufikisha elimu na taarifa wlizopata juu ya upimaji wa Saratani ulionzishwa na hospitali ya Agakhan.

“Hospitali ya Agakhan imeanzisha Kampeni hii Maalumu ili kuweza kuwasaidia wakinamama wote wenye uwezo wakati, wachini na wasio na uwezo kwa kutumia vigezo walivyonavyo na kwa gharama nafuu inayojumuisha Uchunguzi wa aina tatu Kupapasa, Picha na Biopsy”, alisema bibi Mwasha.

 “Tunaunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha huduma za afya kwa jamii nchini kwa watu wote”, alisisitiza Bibi. Mwasha.

Huduma hizi zinatolewa kwa ujumla yaani (package) ili kuwawezesha kinamama kupata huduma ya upimaji. Kampeni hii ya Upimaji wa Saratani tayari imeshafanyika katika mikoa ya Mwanza, Mtwara, Lindi na tutaendelea na kampeni hii katika mikoa na mbalimbali haa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...