Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa kuamkia leo ametunuku nishani na Tuzo kwa viongozi mbalimbali wa kitaifa na watumishi wa umma wapatao 86 waliotoa mchango wao katika kuulinda na kuudumisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliodumu kwa miaka Hamsini 50.
Mama Maria Nyerere akipokea nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano(Order) kwa niaba ya Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Mama Maria Nyerere Nishani ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungnao Daraja nne.

Mama Fatma Karume akipokea Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano(Order) kwa niaba ya Marehemu Abeid Aman Karume Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Mama Fatma Karume nishani ya kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano Daraja Nne wakati wa hafla ya kutunuku nishani na tuzo za miaka 50 Muungano zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano ikulu jijini Dar es Salaam jana usiku.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Rais mstaafu wa Awamu ya tatu Mh.Benjamin William Mkapa Nishani ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano(Order) wakati wa sherehe ya kutunuku nishani na tuzo iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano ikulu jijini Dar es Salaam jana usiku.(picha na Freddy Maro)
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Nishani ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Kwanza Waziri Mkuu mstaafu ambaye pia alikuwa Mwenyekiti Tume ya kurekebisha Katiba  Mhe. JajiJoseph Sinde Warioba wakati wa Sherehe hizo zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano ikulu jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia jana Picha zote na Freddy Maro



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. warioba hongera jk kwa kutokuwa na nongwa

    ReplyDelete
  2. Mzee Ruhusa alikuwa wapi?

    ReplyDelete
  3. tunaomba listi ya wote walipewa hii nishati

    ReplyDelete
  4. Mama Karume, ningekuwa mjengoni hapo ningekuongezea na Fulana ya Yanga SC kama zawadi ya malezi bora kwenye michezo!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...