MAREHEMU BALOZI FULGENCE MICHAEL KAZAURA
Familia ya Marehemu Balozi Fulgence Michael Kazaura, inapenda kutoa shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa, marafiki na majirani wote ambao tumeshirikiana katika kipindi chote cha kumuuguza Mpendwa wetu Marehemu Balozi Fulgence Michael Kazaura hadi kifo chake kilichotokea tarehe 22 Februari, 2014 huko Chennai, India. Hii imetupa faraja kubwa sana wana Familia katika kipindi hiki kigumu.
Kwa namna ya pekee, Familia inatoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais, Mheshimiwa Dr. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda, Rais Mstaafu, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, Mawaziri Wakuu wastaafu, Mheshimiwa Jaji Joseph Sinde Warioba, Mheshimiwa Edward Lowassa na Mheshimiwa Frederick Sumaye. Shukrani pia ziwaendee Jaji Mkuu Mheshimiwa Mohamed Chande Othman .
Waheshimiwa Mawaziri, Katibu Mkuu Kiongozi Mheshimiwa Balozi Ombeni Sefue, Katibu Mkuu Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt Richard Sezibera, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Said Mecky Sadick, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu Fabian Massawe, Viongozi wa Serikali wastaafu, Viongozi wa vyama vya Siasa, Mabalozi na Wawakilishi wa Nchi mbalimbali hususan Balozi wa Tanzania nchini India.
Vilevile, Familia inapenda kuwashukuru Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Balozi Nicolas Kuhanga, Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Rwekaza Mukandala, Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi wa Taasisi zifuatazo: Benki ya Afrika (BOA), Shirika la Ugavi wa Umeme (TANESCO), Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Centre for Diseases Control (CDC), Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Benki ya Standard Chartered, Benki ya Barclays Tanzania na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) ,
Tunazishukuru pia Taasisi zifuatazo: Wakala wa Huduma za Ndege za Serikali Tanzania, Chama cha Mabalozi Wastaafu Tanzania, Chama cha Maskauti Tanzania, , na Wanachama wa British Legion.
Mahsusi, Familia inawashukuru sana Mhashamu Methodius Kilaini Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, , Paroko wa Kanisa la Mtakatifu Petro, Paroko wa Mugana, Mapadre, Masista na Watawa, kwa kuendesha ibada za Misa, Dar es Salaam na Kijijini Bugandika.
Kwa namna ya pekee pia tunawashukuru Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Kansa Ocean Road, Hospitali ya Misheni Mikocheni, Taasisi ya Kansa ya Apollo, India. Vile vile wana Jumuiya ya Mtakatifu Cecilia, Kwaya ya Jumuiya ya Mtakatifu Cecilia ya Kanisa la Mt Petro, Oysterbay Dar es salaam, na Kwaya ya Parokia ya Mugana, Bukoba.
Kwa vile si rahisi kuwataja wote walioshirikiana nasi katika kipindi hiki cha Msiba, kwa taarifa hii tunawaomba wote kupokea shukrani zetu za dhati kwa moyo wa upendo mkubwa mlioonyesha kwetu.
Tunapenda pia kuwataarifu kuwa kutakuwa na Ibada ya Shukrani itakayofanyika siku ya Jumamosi tarehe 5 April, 2014, katika Kanisa la Mt. Petro Oysterbay, saa nne kamili asubuhi ambayo itafuatiwa na chakula cha mchana nyumbani kwa Marehemu, Mtaa wa Guinea, Nyumba No. B.3-1, TIRDO Estate, Oysterbay, saa sita kamili mchana. Karibuni sana.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI, APUMZIKE KWA AMANI. AMINA
Mungu mwingi wa rehema ailaze roho ya marehemu mzee wetu mahali pema peponi. Amina
ReplyDelete