KATIKA TUKIO LA
KWANZA:
MTOTO ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA VANESA
PATRICK NJOJO (03) MKAZI WA
ISISI, WILAYANI MBARALI ALIUAWA KWA KUPIGWA NGUMI NA BABA YAKE MZAZI AITWAYE PATRICK
NJOJO (23) MKAZI WA
ISISI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 26.04.2014 MAJIRA YA SAA 23:45
USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA ISISI, KATA NA TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA
MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILI ULEVI WA POMBE ZA KIENYEJI WA BABA
HUYO. MTUHUMIWA AMEKAMATWA, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA
WILAYA MBARALI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA
POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO
KWA JAMII KUEPUKA ULEVI KWANI NI HATARI KWA AFYA ZAO NA UNA MADHARA KATIKA
JAMII. AIDHA ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWAFUNDISHA WATOTO WAO KWA
UTARATIBU MZURI ILI KUEPUKA MATATIZO.
KATIKA TUKIO LA
PILI:
MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 4
– 5 ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FESTO MBIGA, MKAZI WA NSALAGA AMEFARIKI DUNIA
PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI SM 9124 AINA YA FAW LILILOKUWA
LIKIENDESHWA NA DEREVA RAMADHANI
MWALYOYO (30) MKAZI WA ILOMBA JIJINI MBEYA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 26.04.2014 MAJIRA YA SAA 14:45
MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA NSALAGA, KATA YA UYOLE, TARAFA YA IYUNGA,
BARABARA KUU YA MBEYA/IRINGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI
KINACHUNGUZWA, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
MTUHUMIWA AMEKAMATWA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA
POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO
KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA NA KUFUATA
SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Huyu mzazi anayepiga mtoto ngumi mpaka anakufa ana matatizo kweli.
ReplyDelete