Sisi watanzania wa Washington DC, Maryland na Virginia pamoja na vizazi vyetu tunapenda kutoa pongezi kwa Serikali yetu ya Tanzania kwa Mchakato mzima wa Katiba mpya unaoendelea.

Tunapenda Kutoa Tamko Rasmi kwa Bunge la Katiba na Serikali kutoa haki ya Uraia kwa Watanzania Wote popote walipo Duniani. Uraia Wa Mtanzania aliezaliwa Tanzania na Kizazi chake usijali hali na mahala alipo Mtanzania Huyo.

Kutokubaguliwa kwetu kwenye swala hili la Haki ya Kuzaliwa na Kuruhusiwa kwa Uraia Pacha kwa Waliozaliwa Tanzania na Vizazi vyao ni muhimu katika kuimarisha nchi, kutoa haki kwa Watanzania wote waliozaliwa Tanzania pamoja na vizazi vyao. Haki ya kuzaliwa  kwa watanzania wote kutaimarisha Zaidi mahusiano kati ya watanzania tulio nje na serikali yetu tukufu.

Watanzania Hapa Washington, DC na tulio nje tumekuwa mbele kuitangaza nchi yetu, kuiwakilisha nchi yetu na kuibeba Bendera ya Tanzania huku nje . Watanzania tumekuwa tukishirikiana na Viongozi wa nchi yetu wanapokuja huku nje kwenye mambo mbalimbali ya kimaendeleo, kijamii na kielimu ili kuhakikisha nchi yetu inasonga mbele.

Watoto wetu waliozaliwa huku nje wamekuwa wakiimba nyimbo ya Taifa la Tanzania wanapokuja viongozi mbali mbali huku na kwenye shughuli mbali mbali za kitaifa na kimataifa ambazo huwa tunaiwakilisha nchi yetu huku ugenini. 

Watanzania wenye uraia wa Tanzania na Wale waliochukua Urai wa Hapa , pamoja na watoto wao waliozaliwa hapa ambao ni Wamarekani kwa kuzaliwa tunajisikia na tunaipenda Tanzania kama wenzetu walioko Marangu au Kimanzichana. Tofauti iliyopo ni kwamba sisi tuko huku na wenzetu wako Biharamulo. Watoto wetu wamezaliwa hapa na Binamu zao wamezaliwa Chalinze.  Sisi sote na watoto wetu ni watanzania na tunataka tutambulike na kuwa na haki sawa.

Watanzania wa Washington DC, tumekuwa tukishirikiana kwa hali na mali na Ubalozi wa Hapa  kuitanganza nchi yetu na kuitetea na kuiletea sifa nzuri Tanzania. Hivi Sasa Ubalozi wetu hapa Unaandaa sherehe za Miaka 50 ya Muungano na Ni sisi Watanzania wa Ughaibuni tutashiriki kwa Moyo Mmoja na nguvu zote kuipeperusha bendera ya Tanzania kwa niaba ya nchi nzima. Watato wetu wataonyesha utamu wa nyimbo ya Taifa la Tanzania. Viongozi wa Taifa watazungumza na watanzania wa hapa na kujadili maendelea na muelekeo wanchi.     Sisi Ni Watanzania.


Tanzania Itajengwa Na Watanzania. Sisi Na Vizazi Vyetu Huku Ughaibuni ni Watanzania.

Iddi Sandaly,

Rais Wa Jumuiya Ya Watanzania , 
Washington DC, Maryland na Virginia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Bunge la Katiba litawapa vipi Uraia kiholela na Watanzania watawapa vipi Uraia kiholela kwa kigezo cha kuzaliwa TANZANIA?

    KUMBUKENI WIZARA YA MAMBO YA NDANI TANZANIA IMEKUWA INASISITIZA MARA KWA MARA YA KUWA ''KIGEZO CHA KUZALIWA TANZANIA'' SIO SABABU YA KUITWA MTANZANIA!

    KWA MSISITIZO HUO WA ''KUZALIWA TANZANIA PEKE YAKE SIO KIGEZO CHA UTANZANIA'' NDIO KAMA VILE MWAKA JANA 2013 TULIENDESHA OPERESHENI KIMBUNGA TUKAWATIMUA WATU WENGI TU WALIOZALIWA TANZANIA KURUDI KWAO BURUNDI, UGANDA NA RWANDA !

    ReplyDelete
  2. Hivi nyie wabeba mabox mna akili kweli?? au vumbi la box linawachanganya? Hivi kweli unaweza kumkana mama yako au baba yako mzazi baada ya kupata utajiri alafu baadae dunia inapokufundisha useme ooops wewe ni mzazi wangu naomba nikuite baba/mama na wewe uniite mtoto???!! Si umeshapata rahana hapo???!!

    Nawashauri wabunge wa bunge maalumu la katiba msiwasikilize hawa watu walioukana uraia wa Tanzania kwa sababu za kutajirika nchini kwengine...Kwanza mkiwapima akili za hawa wabeba mabox utawakuta zaidi ya nusu wako demented and stressed so hawajui wanacho ongea.

    Pia viongozi husika kamwe msije kufanya maamuzi kisa tu eti watoto, ndugu zenu wana uraia nje!

    Mbona mimi nimesoma nje from scratch and stayed kama miaka 12 na kuzaa nje lakini mtoto wangu nilimpa passport ya Tanzania na kamwe sijawahi kuukana Utanzania wangu ingawa nilikuwa na nafasi baada ya miaka 5 ya kwanza kuomba uraia wa nje!! Na sasa nipo Tanzania na maisha yanaenda. Nyie mbona mnashindwa kwa kupenda shortcut ya maisha?!.

    Wizara ya mambo ya ndani, TISS, Wizara ya ulinzi na wizara zingine angalieni ili swala kiundani kabla hatujajenga ukuta. Angalieni nchi inapokwenda na sio maslahi ya watoto wenu, ndugu, marafiki zenu maana hatutaki wanyarwanda, Malawi, nk kuja kutudhuru hapo baadae.

    Ankal, naomba usiibanoe hii msg kwa manufaa ya nchi yetu.

    Asanteni.

    ReplyDelete
  3. Mlitoka tanzania.mkaenda nje.mkajifanya mmekimbia vita rwanda na somalia.mkapewa vibali vya kuishi km wakimbizi wa somalia au rwanda.baadae mkapata uraia wa nchi mlizopo mfn marekani sasa mnataka kurudi kua raia wa tanzania lkn hamtaki kuacha uraia wa marekani.its obvious mnataka vyote.na mnataka mawili moja humponyoka.so ndugu zetu chagueni moja.No hard feelings just my opinion.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...