Sisi
watanzania wa Washington DC, Maryland na Virginia pamoja na vizazi vyetu
tunapenda kutoa pongezi kwa Serikali yetu ya Tanzania kwa Mchakato mzima wa
Katiba mpya unaoendelea.
Tunapenda
Kutoa Tamko Rasmi kwa Bunge la Katiba na Serikali kutoa haki ya Uraia kwa
Watanzania Wote popote walipo Duniani. Uraia Wa Mtanzania aliezaliwa Tanzania na
Kizazi chake usijali hali na mahala alipo Mtanzania Huyo.
Kutokubaguliwa
kwetu kwenye swala hili la Haki ya Kuzaliwa na Kuruhusiwa kwa Uraia Pacha kwa
Waliozaliwa Tanzania na Vizazi vyao ni muhimu katika kuimarisha nchi, kutoa
haki kwa Watanzania wote waliozaliwa Tanzania pamoja na vizazi vyao. Haki ya
kuzaliwa kwa watanzania wote kutaimarisha
Zaidi mahusiano kati ya watanzania tulio nje na serikali yetu tukufu.
Watanzania
Hapa Washington ,
DC na tulio nje tumekuwa mbele kuitangaza nchi yetu, kuiwakilisha nchi yetu na
kuibeba Bendera ya Tanzania
huku nje . Watanzania tumekuwa tukishirikiana na Viongozi wa nchi yetu wanapokuja
huku nje kwenye mambo mbalimbali ya kimaendeleo, kijamii na kielimu ili
kuhakikisha nchi yetu inasonga mbele.
Watoto
wetu waliozaliwa huku nje wamekuwa wakiimba nyimbo ya Taifa la Tanzania
wanapokuja viongozi mbali mbali huku na kwenye shughuli mbali mbali za kitaifa
na kimataifa ambazo huwa tunaiwakilisha nchi yetu huku ugenini.
Watanzania
wenye uraia wa Tanzania na Wale waliochukua Urai wa Hapa , pamoja na watoto wao
waliozaliwa hapa ambao ni Wamarekani kwa kuzaliwa tunajisikia na tunaipenda
Tanzania kama wenzetu walioko Marangu au Kimanzichana. Tofauti iliyopo ni
kwamba sisi tuko huku na wenzetu wako Biharamulo. Watoto wetu wamezaliwa hapa
na Binamu zao wamezaliwa Chalinze. Sisi
sote na watoto wetu ni watanzania na tunataka tutambulike na kuwa na haki sawa.
Watanzania
wa Washington DC, tumekuwa tukishirikiana kwa hali na mali na Ubalozi wa Hapa kuitanganza nchi yetu na kuitetea na kuiletea
sifa nzuri Tanzania. Hivi Sasa Ubalozi wetu hapa Unaandaa sherehe za Miaka 50
ya Muungano na Ni sisi Watanzania wa Ughaibuni tutashiriki kwa Moyo Mmoja na
nguvu zote kuipeperusha bendera ya Tanzania kwa niaba ya nchi nzima.
Watato wetu wataonyesha utamu wa nyimbo ya Taifa la Tanzania . Viongozi wa Taifa
watazungumza na watanzania wa hapa na kujadili maendelea na muelekeo wanchi. Sisi
Ni Watanzania.
Iddi Sandaly,
Rais Wa Jumuiya Ya
Watanzania ,
Washington DC , Maryland
na Virginia.
Bunge la Katiba litawapa vipi Uraia kiholela na Watanzania watawapa vipi Uraia kiholela kwa kigezo cha kuzaliwa TANZANIA?
ReplyDeleteKUMBUKENI WIZARA YA MAMBO YA NDANI TANZANIA IMEKUWA INASISITIZA MARA KWA MARA YA KUWA ''KIGEZO CHA KUZALIWA TANZANIA'' SIO SABABU YA KUITWA MTANZANIA!
KWA MSISITIZO HUO WA ''KUZALIWA TANZANIA PEKE YAKE SIO KIGEZO CHA UTANZANIA'' NDIO KAMA VILE MWAKA JANA 2013 TULIENDESHA OPERESHENI KIMBUNGA TUKAWATIMUA WATU WENGI TU WALIOZALIWA TANZANIA KURUDI KWAO BURUNDI, UGANDA NA RWANDA !
Hivi nyie wabeba mabox mna akili kweli?? au vumbi la box linawachanganya? Hivi kweli unaweza kumkana mama yako au baba yako mzazi baada ya kupata utajiri alafu baadae dunia inapokufundisha useme ooops wewe ni mzazi wangu naomba nikuite baba/mama na wewe uniite mtoto???!! Si umeshapata rahana hapo???!!
ReplyDeleteNawashauri wabunge wa bunge maalumu la katiba msiwasikilize hawa watu walioukana uraia wa Tanzania kwa sababu za kutajirika nchini kwengine...Kwanza mkiwapima akili za hawa wabeba mabox utawakuta zaidi ya nusu wako demented and stressed so hawajui wanacho ongea.
Pia viongozi husika kamwe msije kufanya maamuzi kisa tu eti watoto, ndugu zenu wana uraia nje!
Mbona mimi nimesoma nje from scratch and stayed kama miaka 12 na kuzaa nje lakini mtoto wangu nilimpa passport ya Tanzania na kamwe sijawahi kuukana Utanzania wangu ingawa nilikuwa na nafasi baada ya miaka 5 ya kwanza kuomba uraia wa nje!! Na sasa nipo Tanzania na maisha yanaenda. Nyie mbona mnashindwa kwa kupenda shortcut ya maisha?!.
Wizara ya mambo ya ndani, TISS, Wizara ya ulinzi na wizara zingine angalieni ili swala kiundani kabla hatujajenga ukuta. Angalieni nchi inapokwenda na sio maslahi ya watoto wenu, ndugu, marafiki zenu maana hatutaki wanyarwanda, Malawi, nk kuja kutudhuru hapo baadae.
Ankal, naomba usiibanoe hii msg kwa manufaa ya nchi yetu.
Asanteni.
Mlitoka tanzania.mkaenda nje.mkajifanya mmekimbia vita rwanda na somalia.mkapewa vibali vya kuishi km wakimbizi wa somalia au rwanda.baadae mkapata uraia wa nchi mlizopo mfn marekani sasa mnataka kurudi kua raia wa tanzania lkn hamtaki kuacha uraia wa marekani.its obvious mnataka vyote.na mnataka mawili moja humponyoka.so ndugu zetu chagueni moja.No hard feelings just my opinion.
ReplyDelete