Timu ya Taifa ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania imetwaa ubingwa wa Dunia wa Watoto wa Mitaani baada ya jana (Aprili 6 mwaka huu) kuilaza Burundi mabao 3-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa jijini Rio de Janeiro, Brazil.

Mshambuliaji Frank William alifunga mabao matatu katika mechi hiyo iliyochezwa uwanja mkongwe na maarufu wa klabu ya Fluminense huku mgeni rasmi akiwa Waziri wa Fedha wa Uingereza, George Osborne.

Tanzania ilipata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuitandika Marekani mabao 6-1 ambapo hadi mapumziko ilikuwa mbele kwa mabao 4-0.

Burundi ilipata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuifunga Pakistan mabao 4-3 katika mechi ya nusu fainali ya pili.

Timu ya Tanzania inarejea nchini Alhamisi (Aprili 10 mwaka huu) ambapo itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 10 jioni kwa ndege ya Emirates.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Ni nchi chache hasa maskini zilizo na watoto wa mitaani kwa hiyo ilikuwa njia nyepesi kuchukua ubingwa!!

    ReplyDelete
  2. Hope is being created to these kids...they now have a chance in life, once more! Congrats to all those who made this a possibility!

    ReplyDelete
  3. watoto wa mitaani wapo dunia nzima tena nchi zilizoendelea huwa wanafanywa vibaya sana.isipokuwa hawa wenzetu huwa wanafanya kama foster mother.

    ReplyDelete
  4. We anom wa kwanza wacha wivu wako.kama ni rahisi kusha basi wangetangazwa wote walioshirili kua mabingwa.
    Hongera vijana mmepeperusha bendera ya nchi yenu ugenini and well done!
    Ankal naomba nim***kane huyu.

    ReplyDelete
  5. @anonymous # 1 Marekani ni nchi masikini?

    ReplyDelete
  6. Naomba TIMU hii ikifika ipelekwe BUNGENI Dodoma. baada ya hapo naomba vijana hawa wawe ni watoto wa taifa yaani wakae kwenye kambi maalum ili tuwalee na kila mechi ya inapochezwa hapa nchini kuwe na asilimia 5 ya mapato kwa kuisaidia Timu hii.

    ReplyDelete
  7. anon wakwanza ni mvivu wa kufikiri kama si ufinyu wa mawazo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...