Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Uongozi wa Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais katika kikao cha utekelezaji Mpango kazi wa Robo tatu ya mwaka Julai-Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Unguja leo asubuhi.
Baadhi ya maafisa wa idara mbali mbali za Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais wakiwa katika kikao cha utekelezaji Mpango kazi wa Robo tatu ya mwaka Julai-Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Unguja leo asubuhi,mwenyekiti wake akiwa ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.(Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.)
Bw. Michuzi huyu reporter wako toka visiwani huwa anatumia neno MAKAMO wa Rais katika maandishi yake siku zote.
ReplyDeleteNeno sahihi ni MAKAMU, hicho ndio kiswahili fasaha.
Na ma editor mnahitajika kufanya marekebisho.
Inakera kidogo kuwa kila siku huyu reporter hutumia hilo neno.