Na. James Katubuka
Timu ya Mpira wa Pete ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma imeendelea kutoa dozi katika michuano ya Mei Mosi 2014 baada ya kuichachafya CDA Dodoma kwa magoli 42 – 15 katika mchezo uliochezwa jana Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Mchezo huo ulikuwa wa aina yake na ushindani wa sababu CDA inaundwa na wachezaji wazoefu katika mashindano ilhali Ofisi ya Rais Utumishi iliundwa na kikosa cha wachezaji ambao wamewahi kucheza katika ya Taifa ya mpira wa Pete miaka iliyopita.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika CDA ilishakubali magoli 16 dhidi ya matano.
Wachezaji walioisaidia Utumishi kugawa dozi hiyo, ambayo ilileta furaha kwa mashabiki wake ni Fatuma Machenga (GA) na Mwadawa Twalibu (GS).
Wengine walikua ni Anna Msulwa (WA) na Elizabeth Fusi (C) waliofanya kazi ya kugawa mmipira iliyozaa magoli.Kocha wa timu ya CDA Dodoma Bi. Susan Nkurlu alisema kuwa mchezo ulikuwa mzuri na wa kuvutia hivyo aliwapongeza wachezaji wote kwa kuonyesha mchezo safi.
“Nimewakosa wachezaji wangu tegemeo hivyo tumefungwa ila tutarudi na nguvu mpya “
Hata hivyo, kocha wa timu ya Ofisi ya Rais, Utumishi Mathew R. Kambona alisema zipo kasoro ambazo atazifanyia kazi ili kuhakikisha ushindi kwa timu yake unakuwa mkubwa zaidi.
Mashindano ya Mei Mosi 2014 yanazikutanisha taasisi mbalimbali za Umma kimichezo na yanafanyika kitaifa mkoani Morogoro.
Mchezaji wa Ofisi ya Rais, Utumishi Lilian Sylidion (GK) akinyaka mpira na kuwazidi wachezaji wa CDA Dodoma katika mechi iliyochezwa jana ya mashindano ya Mei Mosi 2014 katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Mchezaji wa CDA ya Dodoma (mwenye mpira) akijianda kutoa pasi kwa huku akiwa kazingirwa na wachezaji wa Utumishi katika mechi iliyochezwa jana katika mashindano ya Mei Mosi 2014 yanayoendelea katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Mwadawa Twalibu (GA) wa timu ya Ofisi ya Rais Utumishi akijiandaa kuchukua mpira licha ya upinzani wa wachezaji wa CDA Dodoma katika mashindano ya Mei Mosi 2014 yanayoendelea katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Mchezaji wa Ofisi ya Rais, Utumishi Sophia Komba (C) akijiandaa kutoa pasi kwa Fatuma Machenga (GS) katika eneo la goli la wapinzani wao CDA Dodoma katika mashindano ya Mei Mosi 2014 yanayoendelea katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Anna Msulwa (WA) wa Ofisi ya Rais, Utumishi akijiandaa kutoa pasi kwa Mwadawa Twalibu (GA) katika mechi iliyochezwa jana dhidi ya CDA Dodoma katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Mchezaji Sophia Komba (C) wa Ofisi ya Rais,Utumishi akijiandaa kutoa pasi kwa Fatuma Machenga (GS) na Mwadawa Twalibu (GA) katika mechi iliyochezwa jana dhidi ya CDA Dodoma ya mashindano ya Mei Mosi 2014 yanayoendelea katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...