Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Samuel Sitta akiangalia vitabu katika maktaba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kabla ya kushuhudia uzinduzi wa kituo cha taarifa katika maktaba hiyo.
Naibu Waziri Wizara ya Fedha Mhe. Adam Malima akiangalia vitabu katika maktaba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kabla ya kushuhudia uzinduzi wa kituo cha taarifa katika maktaba hiyo.
Mawaziri kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaoshughulikia masuala ya Jumuiya wakiwa wakipitia machapisho mbalimbali katika maktaba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kabla ya kushuhudia uzinduzi wa kituo cha taarifa katika maktaba hiyo.
Waziri Sitta akioneshwa mkataba wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyovunjika mwaka 1977.
Waziri Sitta akiongea na vyombo vya habari mara baada ya uzinduzi wa kituo cha taarifa katika maktaba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...