.Kiongozi wa Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa 47 wa Tume ya Idadi ya Watu na Maendeleo, Bw. Charles Pallangyo, Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, akizungumza wakati wa majadiliano ya jumla kuhusu mada kuu ya mkutano huu wa siku tano kuhusu tathmini ya utekelezaji wa Mapango wa Utekelezaji wa Mkutano wa Kimataifa juu ya Idadi ya Watu na Maendeleo (ICPD) uliofanyika mwaka 1994 huko Cairo, Misri. Wanaooneka nyuma ni Bw. Noel Kaganda, Afisa wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, na Bw. Stephen Kiberiti -Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.Tanzania ni kati ya nchi 47 zinazounda Tume ya Idadi ya Watu na Maendeleo.
Sehemu ya wajumbe wanaoziwakilisha serikali zao katika mkutano huu. Pamoja na wawakilishi wa serikali, mkutano huu pia kutokana na umuhimu wa mada yenyewe unahudhuriwa na idadi kubwa wajumbe kutoka Asasi zisizo za kiserikali.
Kutoka na uwingi wa wajumbe na hivyo kuufanya ukumbi wa mkutano kuwafinyu, wajumbe wengine walilazimika kufuatilia majadiliano kwa kuangalia kwenye screen katika ukumbi mwingine ( overflow room) kama wanavyooneka sehemu ya ujumbe wa Tanzania, kutoka kulia ni Bi. Samia A. Diria, Afisa, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Ngasuma Kanyeka ( International Parenthood) Bw. Enock A. Mhehe, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Bi. Vanessa Anyoti ( YWCA)
Wajumbe wengine wa Tanzania kutoka kushoto. Bw. Edwin M. Minde kutoka Ofisi ya Rais Tume ya Mipango, Bi. Lulu Ng'wanakilala ( UMATI) Dkt. Mohameed Dahoma, Mkurugenzi wa Huduma za Kinga na Elimu ya Afya, Wizara ya Afya -Zanzibar na mjumbe wa mwisho kutoka United Nations Association. Ujumbe huu wa Tanzania ulikuwa ukishiriki katika majadiliano ya maandalizi ya Azimio la Mkutano huu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...