Mtaalamu kutoka TASAF Makao makuu Bi. Mercy Mandawa Mariki mwenye miwani na kompyuta mpakato akiandika baadhi ya mambo yaliyojitokeza kwenye mafunzo ya wawezeshaji ngazi ya wilaya mjini Dodoma.
 Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya namna ya kuendesha kazi yautambuzi wa kaya masikini ngazi ya halmashauri ya wilaya wakimsikiliza mtoa mada hayupo pichani katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Dodoma.
 Mtoa mada katika mafunzo ya wawezeshaji ngazi ya Wilaya, Bw. Andrew Kibona akitoa mada kwenye mafunmzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa shule ya sekondari ya Dodoma.
Washiriki wa mafunzo ya uwezeshaji wa mpango wa kunusuru kaya masikini katika manispaa ya Dodoma wakimsikiliza mtoa mada hayupo pichani juu ya namna ya kuzitambua kaya masikini .

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii,TASAF uimeanza  utekelezaji wa Mpango wa  kunusuru kaya masikini katika mikoa ya Dodoma, Singida ,Kigoma na Katavi ambako mafunzo kwa wawezeshaji wa Mpango huo ngazi ya halmashauri za wilaya yameanza kutolewa.

Mpango huo utakaotekelezwa nchini kote kwa awamu, tayari umekamilika katika mikoa ya Lindi na Mtwara ambako kaya masikini zitaanza kupatiwa ruzuku kwa ajili ya kuboresha afya kwa mama wajawazito na watoto wenyer umnri wa  chini ya miaka 5, na kuziwezesha kaya husika kumudu gharama za elimu na matibabu kwa familia husika ili kuboresha maisha yao.

Ruzuku hiyo ya fedha pia  inakusudiwa kuzijengea uwezo kaya masikini ziweze kuinua kipato  kwa kuanzisha shughuli za kiuchumi kulingana na mazingira ya eneo husika ili hatiomaye ziweze kuondokana na umasikini wa kipato.

Akizungumza katika mkutano wa wawezeshaji ngazi ya taifa  mjini Dodoma, Bi Mercy Mandao amehimiza umuhimu wa kuendesha zoezi zima la utanmbuzi wa kaya masikini kwa uangalifu mkubwa ili hatimaye walengwa waweze kupatikana na kuondoa uwezekano wa kuwaacha walengwa kutokana na kutozingatia vigezo maalumu ambavyo huwekwa na wananchi wenyewe kwenye maeneo yao.

Zifiatazo ni picha za baadhi ya washiriki wa mafunzo ya wawezeshaji  katika manispaa  ya Dodoma yaliyoanza leo Jumanne . Mafunzo kaya hao yatolewa pia katika halmashauri zote za mikoa ya Singida, Kigoma, Katavi, Rukwa ,na Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...