Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akizungumza na wanamichezo wanaoenda kuweka kambi katika nchi za New Zealand, Ethiopia, China na Uturuki ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya Jumuiya ya Madola mapema mwezi julai. Kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leornard Thadeo.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leornard Thadeo akifafanua jambo wakati wa hafla ya kuwakabidhi bendera wanamichezo wanaokwenda nje ya nchi kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Jumuiya ya Madola leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya njeya nchi na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe (wa tatu kutoka kushoto) akifurahia mara baada ya kuwa kabidhi Bendera ya Taifa wawakilishi wa wanamichezo wanaokwenda nchini New Zealand, Ethiopia,China na Uturuki kwa ajili ya kujiandaa na msahindano ya Jumuiya ya Madola. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Masuala ya Asia, Balozi Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Leornard Thadeo, Katibu wa Kamati ya Olympic Tanzania Filbert Bayi na mwakilishi wa wana michezo Neema Mwaisyula.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...