Mwandishi wa kitabu kinachoelezea namna watanzania na makampuni ya usambazaji ya hapa Tanzania yanavyoweza kushiriki, kuwezeshwa na kunufaika na sekta ya nishati ya gesi asilia hapa.Bi. Neema Lugangilra Apson akielezea maudhui ya Kitabu chake kwa wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kitabu chake jana usiku jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu kinachoeleza namna watanzania na makampuni ya usambazaji yanavyoweza kushiriki, kuwezeshwa na kunufaika na sekta ya nishati ya gesi asilia hapa. Kulia ni mwandishi wa kitabu hicho Bi. Neema Lugangilra Apson.
Bi. Neema Lugangilra Apson akionesha kitabu chake kinachoitwa “Local Content in Supplier Development” kinachoelezea namna watanzania na makampuni ya usambazaji yanavyoweza kushiriki, kuwezeshwa na kunufaika na sekta ya nishati ya gesi asilia hapa.
Mgeni Rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akipokea kitabu kinachoelezea namna watanzania wanavyoweza kushiriki na kunufaika na sekta ya nishati ya gesi asilia hapa nchini. Kulia ni mwandishi wa kitabu hicho Bi. Neema Lugangilra Apson.
Tunashukuru kwa taarifa hii na asante zimwendee mwandishi kwa kazi nzuri na utashi wa kuielimisha jamii yetu. Mbali na hapo ningeomba mwandishi atupatie mawasiliano zaidi ya jinsi ya kuweza kupata nakala ya kitabu hiki. Vile vile, Je hakuna uwezekano wa kupata eleckronic copy ya kitabu hiki? Nadhani ingekuwa rahisi zaidi kama maarifa haya yangetolewa pia kwa njia hiyo kutokana na urahisi utakao pelekea watu wengi kuyapata maarifa hayo. Mdau Texas.
ReplyDelete