Na John Gagarini, Kibaha


MKAZI wa Ruaha mkoani Morogoro Sibeteli (34) anashikiliwa na jeshi la Polisi mkoani Pwani kwa tuhuma za kukutwa na vipande 28 vya meno ya tembo ambavyo ni nyara za serikali.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa ameyahifadhi meno hayo ndani ya gari aina ya Toyota Mark II yenye namba za usajili T 129 ARH.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kaimu kamanda wa polisi mkoani Pwani Kamishna Msaidizi (ACP) Steven Kiango alisema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 22 mwaka huu majira ya saa 1:30 usiku eneo la kijiji cha Vigwaza kata ya Vigwaza Tarafa ya Chalinze wilaya ya Bagamoyo.

Kamanda Kiango alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa na askari ambao walikuwa doria  ambapo ilibainika kuwa alitoka Mikumi kuelekea Dar es Salaam.

Aidha alisema kuwa mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara upelelezi wa tukio hilo utakapokamilika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...