Pichani Kati ni Mwenyekiti wa CHADEMA kata ya Shati,Wilayani Iramba,Bwa Ezekiel Makala akionesha kadi yake na kutangaza kujiunga na chama cha CCM,kwenye mkutano wa hadahara uliofanyika kwenye stendi ya mabasi ya Kiomboi,wilayani Iramba mkoani Singida,shoto ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na kulia ni Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi na Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Mwigulu Nchemba wakishuhudia kwa pamoaja.
Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikad,siasa na Uenezi Nape Nnauye,katika ziara ya Kukagua kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Chama,kukagua maandalizi ya uchaguzi ya serikali za mitaa,kusikiliza kero za wananchi na kuzitafututia ufumbuzi.
Pichani Kati ni Mwenyekiti wa CHADEMA kata ya Shati,Wilayani Iramba,Bwa Ezekiel Makala pamoja na Katibu wake Bwa.Joseph Kingu wakitangaza kutangaza kujiunga na chama cha CCM,kwenye mkutano wa hadahara uliofanyika kwenye stendi ya mabasi ya Kiomboi,wilayani Iramba mkoani Singida,Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na kulia ni Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi na Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Mwigulu Nchemba wakishuhudia kwa pamoja.
Mwenyekiti wa CHADEMA kata ya Shati,Wilayani Iramba,Bwa Ezekiel Makala pamoja na Katibu wake Bwa.Joseph Kingu sambamba na wanachama wengine kutoka chama hicho cha CHADEMA,Bwa.Ayoub Gofrey kutoka kata ya Makunde,Julius Kizanda kata ya Mtekente na Ally Saleh kata ya Kisila wakila kiapo cha utii mara baada ya kutangaza rasmia kuachia ngazi nafasi zao na kuhamia chama cha CCM,kwenye mkutano wa hadahara uliofanyika leo jioni kwenye stendi ya mabasi ya Kiomboi,wilayani Iramba mkoani Singida.
Viongozi hao wa CHADEMA walikiri wazi kwenye mkutano wa hadhara kuwa chama cha CCM,ndicho chama bora na kitaendelea kutokuwa na mpinzani siku hadi siku,kwa sababu kinaonesha nia ya dhati ya kuwa karibu na wananchi ikiwemo na kuwasikiliza na kuwatatulia matatizo yao.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma orodha ya vijiji
vitakavyopata umeme katika Wilaya ya Iramba,jioni ya leo kwenye mkutano
wa hadhara uliofanyika Shelui mkoani Singida.
Wananchi
wa Kiomboi wakishangilia jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM,Nugu Kinana
alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara jioni leo katika stendi ya
mabasi ya Kiomboi,Wilayani Iramba mkoani Singida.
Katibu
wa NEC,Itikadi Siasa na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia kwenye mkutano
wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika stendi ya mabasi ya
Kiomboi,Wilayani Iramba mkoani Singida.
Mbunge
wa Jimbo la Iramba Magharibi na Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Mwigulu
Nchemba akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
jioni ya leo katika stendi ya mabasi ya Kiomboi,Wilayani Iramba mkoani
Singida.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...