Mwimbaji Mahiri wa muziki wa nyimbo za Kiroho a.k.a Injili,Rose Muhando akiimba wimbo wake mpya wa Facebook na Twitter mbele ya mashabiki wake,katika uwanja wa Kambarage mapema jioni ya leo mkoani Shinyanga,ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa tamasha la Pasaka.Tamasha hilo linaloandaliwa na Msama Promotions Ltd kesho jumapili linaendelea katika uwanja wa CCM Kirumba jijiini Mwanza,ambapo Nyota wa Nyimbo za Injili kutoka nchini Afrika Kusini,Rebecca Malope atawatumbuiza wakazi wa jiji hilo sambamba na waimbaji wengine..
Mwimbaji wa nyimbo za Injili,Upendo Kilahiro akiimba mbele ya wapenzi wa muziki wa injili ndani ya uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Sehemu ya wapenzi wa muziki wa injili wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo.
Upendo Nkone,ambaye amejizolea sifa kubwa kwa kuimba nyimbo za kusifu na kuabudu,akiwaimbisha mashabiki ba wapenzi wa muziki wa injili ndani ya uwanja wa kambarage jioni ya leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...