Tingatinga la Mamraka ya ustawishaji makao makuu [CDA] likibomoa moja ya nyumba zilizopo katika hifadhi ya Barabara inayotarajiwa kuanza kujengwa havi karibuni, ambapo zaidi ya nyumba 65 zilibomolewa katika eneo hilo la mlamwa kusini.

 Wanawake wa mtaa wa Mlimwa wakimsaidia Mwenzao aliyezirai baada ya Tingatinga la CDA kufika kwa ajili ya kubomoa nyumba yake kwa ajili ya kupisha ujenzi wa Barabara, zoezi hilo lilifanyika Jana ambapo nyumba zaidi ya 65 zilibomolewa na kuacha familia zaidi ya 150 zikikosa makazi.
 Mwenyekiti wa mtaa huo Zubeda Haji akielekeza jambo wakati wa ubomoaji huo.
 Wananchi wa Mlimwa waking'oa mabati muda mfupi kabla ya Tinga tinga la CDA kufika na kuibomoa nyumba hiyo ili kupisha hifadhi ya Barabara
  Bibi huyu mkazi wa Mlimwa Kusini ambaye hakufahamika jina lake akiwa hajui la kufanya baada ya nyumba yake aliyokuwa akiishi iliyojengwa kwa mtindo wa Tembe huku akiachwa na vyombo vyake alivyoweka kwenye shamba la mahindi baada ya CDA kufanya uvunjaji huo kwa nyumba zote zilizopo katika hifadhi ya Barabara.
Wananchi wa Mlimwa kusini wakiwa katika hekaheka ya kuhamisha mizigo yao na kukimbia nyumba zao baada ya kupata taarifa za ujio wa Tinga tinga la CDA kwa ajili ya kubomoa nyumba zao ili kupisha ujenzi wa barabara.PICHA NA JOHN BANDA WA PAMOJA BLOG

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...