Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM, Prof. Idris Kikula mwishoni mwa wiki alifunga BONANZA la michezo mbalimbali iliyofanyika chuoni hapo kwa muda wa wiki moja.

Michezo hiyo ilifadhiliwa na mfuko wa mafao ya Jamii PPF ambapo ilikutanisha timu mbali mbali katika mpira wa pete na mguu.

Timu zilizoshiriki zilikuwa nane,timu kutoka School saba na timu kutoka Utawala moja.Pamoja na mpira wa Pete na Miguu kulikuwepo mashindano ya kuvuta kamba na kukimbiza kuku,Katika siku ya kufunga mashindano hayo.

Mfuko wa hifadhi ya jamii PPFwaliwakilishwa na Bwana Julius S.Shayo mwakilishi wa kanda ya kati. Katika bonanza hilo ambalo pamoja na kufadhili walitoa mbali mbali ikiwamo vikombe kwa washindi pamoja na fedha taslimu.

Washindi katika Mpira wa miguu amao fainali zilikutana timu kutoka Shule(School)ya Sayansi Asilia na Hesabu na Chuo cha Sayansi Jamii washindi walikuwa Sayansi Asilia ambao walivalia Jezi nyeupe walipata ushindi wa goli sita kwa goli tano.

Kwa upande wa Mpira wa Pete Ulio kutanisha timu za Shule(School) Elimu na Shule Sayansi Jamii na Elimu Angavu Washindi walikuwa Shule ya Elimu kwa jumla ya vikapu 26 kwa 16.
Mwalilishi wa PPF Kanda ya Kati Ndugu Julius S Shayo akimkaribisha Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Prof.Idris Kikula (kulia) wakati wa kufunga tamasha la michezo Boanza la wiki moja lililo kuwa limefadhiliwa na mfuko huo.
Pror.Idris Kikula akagua kikosi cha timu ya Sayansi asilia na Hesabu.
Kikosi kamili cha timu ya Sayansi asilia na Hesabu(ndani ya jezi nyeupe) kikiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Kikosi cha timu ya Sayansi Jamii kikiwa katika picha ya pamoja.
Kikosi cha Shule ya Sayansi ya mawasiliano na Elimu Angavu kikiwa katika jezi ya blue na mgeni rasimi.
Washindi wa pete kikosi cha Elimu. Picha na Deusdedit Moshi wa Globu ya Jamii Kanda ya Kati Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 05, 2014

    Jamani mwandishi una hakika na hilo jina la VC wa UDOM? si vizuri kukosea majina ya watu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...