TAARIFA ZILIZOIFIKIWA GLOBU YA JAMII USIKU HUU,ZINAELEZA KUWA ALIEKUWA MUONGOZAJI WA FILAMU NA VIPINDI MBALI MBALI VYA TELEVISHENI HAPA NCHINI,GEORGE TYSON (PICHANI), AMEFARIKI DUNIA.
GEORGE TYSON AMEFIKWA NA MAUTI HAYO USIKU HUU BAADA YA KUPATA AJALI MBAYA SANA BAADA YA  GARI WALIOLOKUWA WAKISAFIRIA KUTOKA MKOANI DODOMA KUJA DAR ES SALAAM, KUPINDUKA MARA KADHAA KUTOKANA NA KUPASUKA MATAIRI YA GARI HIYO AINA YA TOYOTA NOAH. 
AJALI HIYO IMETOKEA MAJIRA YA SAA MOJA JIONI,ENEO LA GAIRO MKOANI MOROGORO.WAALIKUWA WAKITOKEA KWENYE HAFLA YA KUADHIMISHA MIAKA MIWILI YA KIPINI CHA TELEVISHENI CHA THE MBONI SHOW.
NDANI YA GARI HILO KULIKUWA NA WATU WANANE AMBAO NAO HALI ZAO NI MBAYA KUTOKANA NA KUUMIA MAENEO MBALI MBALI YA MIILI YAO.  WOTE WALIKIMBIZWA  HOSPITALI YA RUFAA YA MOROGORO KWA MATIBABU.
MAREHEMU TYSON ATAKUMBUKWA KAMA MMOJA WA WATAALAMU WALIOLETA MABADILIKO MAKUBWA KATIKA  TASNIA YA FILAMU NA TV  NCHINI, AKIONGOZA FILAMU NA VIPINDI VINGI VILIVYOPATA MAFANIKIO MAKUBWA. 
ALIKUWA MUME WA MSANII YVONNE CHERRY 'MONALISA' AMBAYE WALIPATA MTOTO WA KIKE, SONIA.
TUTAENDELEA KUPEANA TAARIFA KADRI ZITAKAVYOKUWA ZIKITUFIKIA.
GLOBU YA JAMII INAUNGANA NA NDUGU, JAMAA NA MARFIKI WA MAREHEMU GEORGE TYSON KATIKA KUOMBOLEZA MSIBA HUU.
MOLA NA AIWEKE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI

AMIN.

Kuona baadhi za habari  
enzi za uhai wa Tyson BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 31, 2014

    Kama utani vile, jumanne hii nilikuwa nae ofisini tuongea. Poleni sana wanafamilia na Poleni sana TV1.

    ReplyDelete
  2. No way to run. R. I. P Tyson

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...