TAARIFA ZILIZOIFIKIWA GLOBU YA JAMII USIKU HUU,ZINAELEZA KUWA ALIEKUWA MUONGOZAJI WA FILAMU NA VIPINDI MBALI MBALI VYA TELEVISHENI HAPA NCHINI,GEORGE TYSON (PICHANI), AMEFARIKI DUNIA.
GEORGE TYSON AMEFIKWA NA MAUTI HAYO USIKU HUU BAADA YA KUPATA AJALI MBAYA SANA BAADA YA GARI WALIOLOKUWA WAKISAFIRIA KUTOKA MKOANI DODOMA KUJA DAR ES SALAAM, KUPINDUKA MARA KADHAA KUTOKANA NA KUPASUKA MATAIRI YA GARI HIYO AINA YA TOYOTA NOAH.
AJALI HIYO IMETOKEA MAJIRA YA SAA MOJA JIONI,ENEO LA GAIRO MKOANI MOROGORO.WAALIKUWA WAKITOKEA KWENYE HAFLA YA KUADHIMISHA MIAKA MIWILI YA KIPINI CHA TELEVISHENI CHA THE MBONI SHOW.
NDANI YA GARI HILO KULIKUWA NA WATU WANANE AMBAO NAO HALI ZAO NI MBAYA KUTOKANA NA KUUMIA MAENEO MBALI MBALI YA MIILI YAO. WOTE WALIKIMBIZWA HOSPITALI YA RUFAA YA MOROGORO KWA MATIBABU.
MAREHEMU TYSON ATAKUMBUKWA KAMA MMOJA WA WATAALAMU WALIOLETA MABADILIKO MAKUBWA KATIKA TASNIA YA FILAMU NA TV NCHINI, AKIONGOZA FILAMU NA VIPINDI VINGI VILIVYOPATA MAFANIKIO MAKUBWA.
ALIKUWA MUME WA MSANII YVONNE CHERRY 'MONALISA' AMBAYE WALIPATA MTOTO WA KIKE, SONIA.

TUTAENDELEA KUPEANA TAARIFA KADRI ZITAKAVYOKUWA ZIKITUFIKIA.
GLOBU YA JAMII INAUNGANA NA NDUGU, JAMAA NA MARFIKI WA MAREHEMU GEORGE TYSON KATIKA KUOMBOLEZA MSIBA HUU.
MOLA NA AIWEKE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI
AMIN.
Kuona baadhi za habari
enzi za uhai wa Tyson BOFYA HAPA

Kama utani vile, jumanne hii nilikuwa nae ofisini tuongea. Poleni sana wanafamilia na Poleni sana TV1.
ReplyDeleteNo way to run. R. I. P Tyson
ReplyDelete