Wananchi wa kijiji cha kibaigwa wamefunga Barabara kuu ya Morogoro kwenda Dodoma usiku huu, kwa madai ya kutaka kupunguzwa Kwa ushuru wa mazao na kuamua kufunga barabara hiyo ili waweze kuonana na uongozi wa juu wa Serikali ili kusikilizwa mahitaji yao ambayo wanadai hayajawahi fanyiwa kazi na viongozi wa Kijiji. 

Kinachoendelea hivi sasa ni Jeshi la Polisi likijaribu kuwatawanya wananchi hao kwa kutumia mabomu ya machozi.

Wananchi hao wamejikusanya kuwatawanya kwa wingi katika eneo hilo huku wakiwa wamewasha moto mkubwa ambao umepelekea kuwaka kwa gari moja lililopo kwenye eneo hilo kutokana na kuzuiliwa na wananchi hao huku wakisema hapiti mtu leo hapa. 

Magari ya kwenda na kurudi kutoka mikoa ya dodoma na mingine ya kanda ya ziwa yamekwama pande zote mbili za barabara kwa zaidi ya saa sasa .Gari moja LA serikali limeharibiwa na wananchi hao.

Globu ya Jamii inaendelea kufuatilia tukio hilo kwa ukaribu kabisa na tutaendelea kuwapa taarifa kadri zinavyotufikia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 05, 2014

    Walichofanya hao wanakijiji ni upuuzi usioweza kuvumilika. Sasa hiyo barabara au watumiaji wake wamewakosea nini hao wanavijiji? Sasa kama wanakijiji wana matatizo yao ni bora wangeandamana hadi kwa mkuu wa wilaya au mkoa lakini hili la kufunga barabara likizoeleka italeta matatizo makubwa. Serikali isisitize na iweke wazi kuwa kufunga barabara ni kosa la jinai na yoyote yule anayefanya hivyo ataadhibiwa hao watu wangekoma, lakini ikiendelea kuwabembeleza kwa ajili ya kupata kura zao itaharibu nchu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...