Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limepitisha Bajeti ya
Wizara ya Ujenzi yenye jumla ya Shilingi 1,219,717,592,000.00 kwa ajili ya
matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2014/15.
Hatua hiyo ya Bunge kupitisha Bajeti hiyo itawezesha
Wizara ya Ujenzi kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi
na kuendeleza Sekta ya Ujenzi hapa nchini.
Akiwasilisha hotuba ya bajeti hiyo jana, Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli (Mb), alieleza kuwa kati ya fedha hizo Shilingi
557,483,563,000.00 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida ambazo zinajumuisha
Shilingi 24,338,319,000.00 za mishahara ya Watumishi (PE), Shilingi
6,944,846,000.00 za matumizi mengineyo (OC) na Shilingi 526,200,400,000.00 kwa
ajili ya Mfuko wa Barabara.
Akifafanua kuhusu bajeti ya Maendeleo iliyotengewa Shilingi
662,234,027,000.00, Mhe. Magufuli ameeleza kuwa, kati ya fedha hizo Shilingi 450,000,000,000.00
ni fedha za ndani za miradi ya maendeleo na Shilingi 212,234,027,000.00 ni
fedha za nje za miradi ya maendeleo.
Wizara ya Ujenzi ina
majukumu yafuatayo, Kusimamia Sera za ujenzi na usalama barabarani, Ujenzi na matengenezo ya barabara, madaraja na
vivuko.
Pamoja na majukumu hayo Wizara pia inasimamia
ukarabati wa majengo ya Serikali, huduma za Ufundi na umeme, kusimamia shughuli
za usajili wa Makandarasi, Wahandisi, Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi,
Usalama barabarani na mazingira katika sekta hiyo.
Pia Wizara inasimamia uboreshaji, utendaji na
uendelezaji wa watumishi wa Wizara pamoja na kusimamia utekelezaji wa majukumu
ya Wakala,Taasisi na Bodi zilizo chini ya Wizara.
Taarifa hii imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikali
Wizara ya Ujenzi
21/05/2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...