Jamii wilayani Chato imeaswa kutambua umuhimu na kuwapeleka watoto kupata chanjo kwenye hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati kwa muda muafaka.
Wito huo umetolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa bodi ya Afya Wilayani Chato Bw. Edward Buhile ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa wiki ya Chanjo iliyofanyika hivi karibuni katika hospitali ya Wilaya ya Chato.
Bw. Buhile amesema kumekuwa na tabia ya wazazi kutokuwapeleka watoto kupata chanjo kitendo ambacho si kizuri kwani chanjo hutolewa bure na serikali kupitia hospitali, vituo vya afya na zahanati.
"Ninawaombeni mulete watoto wenu wapate chanjo, tena ni bure kabisa ili tuweze kuwaepusha na magonjwa hatari na Hatimaye kupoteza maisha ya watoto wetu” alisistiza Bw. Buhile.
Katika uzinduzi huo pia Mkuu wa kliniki ya watoto Wilayani Chato Bibi Mary Basiga amewaasa wanaume kuambatana na wake zao pindi wanapohudhuria kliniki ili waweze kujua maendeleo ya mtoto na kumsaidia mama wakati akiwa kliniki ambapo jukumu la kupeleka watoto hivi sasa limeachwa kwa akina mama pekee.
Walengwa wa chanjo ni watoto wenye umri chini ya miaka miwili ambao hawakupata au hawajakalisha chanjo .
Magonjwa ambayo yanakingwa na chanjo nchini Tanzania kwa sasa ni ni kifua kikuu, Dondakoo, Kifaduro, Pilio, Surua, Pepopunda, Homa ya ini, homa ya uti wa mgongo, kichomi na kuhara.
Kwa mwaka 2013 jumla ya watoto 77,824 walipata chanjo mbalimbali wilayani Chato na mwaka huu zaidi ya watoto 80,000 wanategemewa kupatiwa chanjo hizo.
Mwenyekiti
wa bodi ya Afya Wilaya ya Chato bw. Edward Buhile akiongea na wananchi wa Chato
mjini waliohuhudhuria kwenye uzinduzi wa
wiki ya Chanjo Wilayani Chato
Mwenyekiti
wa bodi ya Afya Wilaya ya Chato bw. Edward Buhile (kulia)akimpa mtoto chanjo ya
kuzuia ugonjwa wa Polio kuashiria
uzinduzi wa Chanjo Wilayani Chato
Mwenyekiti
wa bodi ya Afya Wilaya ya Chato bw. Edward Buhile akifurahia jambo na mtoto
aliyepewa chanjo
Baadhi
ya wakazi wa Chato mjini waliohudhuria kwenye uzinduzi wa wiki ya Chanjo
Wilayani Chato
Mkuu
wa Kliniki ya Watoto Bibi. Mary Basiga akifafanua jambo kwa wananchi kuhusu
umuhimu wa Chanjo.
Habari na picha na Richard Kagembe
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...