Mamlaka ya Hali
ya Hewa nchini inapenda kukanusha kuhusiana na taarifa ya ujumbe mfupi wa simu
na katika mitandao ya kijamii wenye maneno yafuatayo : ‘TMA warning heavy rains of strong easterly
winds 100km an hour expected to hit Dar coast from Somalia, Heavy rains 120mm
above sea level expected today and tommorrow. People must avoid Sea and areas
near to Sea should be alert cautioned. Tanzania Meteorological Agency www.tma.gov.tz’
Mamlaka inapenda
kuutaarifu umma kuwa taarifa hiyo siyo ya kweli na ina lengo la kupotosha umma na wala haijatolewa na
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.
Mamlaka ina
kuwakumbusha wananchi wote kuendelea kufuatilia taarifa zetu kupitia vyanzo
husika vya Mamlaka vikiwemo utabiri wa kila siku utolewao kupitia radio, televisheni
na tovuti ya Mamlaka (www.meteo.go.tz).
Taarifa sahihi za mwenendo wa mvua na
tahadhari za hali mbaya ya hewa zinatolewa
na zinapatikana kupitia njia rasmi za utoaji taarifa maalum za kiofisi
(official weather statement).
Hivyo taarifa kuhusiana na mvua
zinazoendelea imekuwa ikitolewa katika utabiri wa kila siku kupitia vyombo vya
habari, mtandao wa kijamii wa Mamlaka na
tovuti ya Mamlaka.
Tunawatakia shughuli njema
katika
ujenzi wa Taifa letu.
IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...