Msanii maarufu na mtumbuizaji Hapa nchini Nassib Abdul, maarufu kama DIAMOND PLATNUMZ,  ni miongoni mwa wasanii waliochaguliwa kwenda katika Tuzo za B.E.T zinazoandaliwa na kituo cha Television cha watu weusi nchini Marekani 'Black Entertainment Television' (BET) Tuzo ambazo zinatambulika sana kimataifa.


Msanii huyu ambae amekuwa nominated kwenye category ya 'Best African Acts' akichuana na wasanii kama Davido (Nigeria), Mafikizolo (Afrika Kusini), Sarkodie (Ghana), na Tiwa Savage (Nigeria). Diamond ambae amekuwa nominated ndio msanii pekee kutoka Africa Mashariki ambae ametangazwa rasmi siku ya Jana katika mtandao wa BET.com.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 14, 2014

    The mdudu,peperusha bendera ya sijui niseme ya Tanganyika au ya Tanzania maana nishachanganyikiwa kabisa na hili swala umati wa watanzania wanataka 3 lakini wachache 2 mm bora niishie hapa ila nataka amani ya nchi yangu na watu wake iwe palepale,nije kwenye mada yangu ya huyu kijana wa Madini ya ajabu yaani Diamond,ikumbukwe wachezaji wa timu ya Taifa stars wameshindwa kuipeperusha bendera ya nchi yetu,wanariadha pia wameshindwa,wangumi pia wameshindwa,ila huyu Dogo hakiyamungu anasitahili pongezi kubwa kwa muda mdogo tu tayari ashaipeperusha vyema nchi yetu KIMATAIFA mm huku UK natembea kwa Mikogo mbele ya Makenya,Minyarwanda,Mirundi, Miganda,so muda ndio huu ndugu zangu tumpigie kula za kumwaga ili awabwage hao wote anaoshindana nao,mwisho kabisa Pongezi kwa jeshi langu la JWTZ kwa kuwang'owa M23 huku UK waafrica wengi washakubari kwamba jeshi letu ni moto wa kuotea mbali,

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 15, 2014

    All the best Diamond and make us proud. An example honest hard work does pay.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 15, 2014

    Piga kazi kijana, ukipata hiyo tuzo ndo tutajua kweli ulistahili hizo 7 za bongo.. TZ HOYEEEE!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 16, 2014

    Kijana anastahili hongera!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...