Mkurugenzi Mkuu wa VODACOM Tanzania Bwana Rene Meza akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam ambapo alizindua Huduma ya M-PAWA leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Huduma ya kampuni ya simu ya VODACOM iitwayo M-PAWA itakayowawezesha watumiaji kutuma na kupokea pesa kwa urahisi zaidi na pia kupata mikopo ya pesa kwa matumizi mbalimbali.Hafla hiyo ya uzinduzi ilifanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam leo.
 Rais Jakaya Kikwete (wa tatu kushoto)akiwa pamoja na kutoka kushoto  Mwenyekiti wa CBA Tanzania Ndewirwa Kitomari, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Vodacom Tanzania Balozi Mwanaidi Maajar, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Rene Meza, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa, Mwenyekiti wa Bodi ya CBA Group Desterio Oyatsi na Naibu Mwenyekiti wa CBA Group Muhoho Kenyatta mara baada ya Rais kuzindua huduma mpya ya M-pawa ya kuweka pesa, kutoa na kukopa kupitia simu ya mkononi kwa njia M-pesa kwa ushirikiano na Benki ya CBA jijini Dar es salaam
Rais Jakaya Kikwete (wa pili kulia) akiwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza  wakifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa huduma ya M PAWA ambayo inamwezesha mteja kupata huduma za kibenki kwenye simu ya mkononi kwa njia ya M-pesa iliyozinduliwa kwa ushirikiano wa Vodacom Tanzania na Benki ya CBA. Kupitia huduma hiyo mteja wa M-pesa anaweza kuweka, kutoa na kukopa pesa.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Huma ya-M-PAWA ya kampuni ya simu ya VODACOM wakisikiliza kwa makini hotuba ya uzinduzi iliyotolewa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo.
Wasanii waionesha mabango wakati wa uzinduzi wa huduma ya M-PAWA.(picha na Freddy Maro)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 15, 2014

    Jamani kwa yeyote anayefahamu zaidi kuhusu kutuma pesa kwa njia ya simu ya mkononi kutoka nje ya nchi. Katolea mfano Mh. Rais kuwa bibi yake anapokea pesa kwa njia ya simu kutoka kwa mwanae london. Mwenye idea namna ya kutuma pesa kwa njia ya simu toka nje naomba ufahamu please. Mtanzania mwema.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 15, 2014

    miamala = transactions
    si utani msamiati mpya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...