Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Naseeb Abdul ‘Diamond’akiongea na waandishi wa habari kabla ya kuanza show hiyo,(kushoto), ni wasanii wa kundi la Sauti Sol.
 Picha ya pamoja.
 Watangazaji wa MTV Base Vanessa Mdee (kushoto),  na Nomuzi Mabe (kulia), wakiwaelezea mashabiki wa muziki kuhusina na show  hizo.
 Kundi la Mi Casa likitoa burudani.
 Diamond akitoa burudani.
  Mashabiki mbalimbali waliofurika katika ukumbi huo wakifuatilia show.
Mashabiki mbalimbali waliofurika katika ukumbi huo wakifuatilia show.

=======  =====  ======
MSANII nyota wa muziki wa kizai kipya nchini Naseeb Abdul ‘Diamond’ ametamba kufanya vizuri katika tuzo za MTV Africa ‘Mama’ zinazotarajiwa kufanyika Juni 7 mwaka huu nchini Afrika Kusini.

Diamond ameingia katika tuzo hizo kwenye vipengele viwili ambavyo ni msanii bora wa Afrika pamoja na msanii mwenye nyimbo bora ya kushirikisha.

Wimbo ambao umembeba kwa kiasi kikubwa msanii huyo ni wa Number One aliomshirikisha Davido wa Nigeria ambapo amewaomba mashabiki wake kumpigia kura kwa wingi.

Akizungumza katika hafla ilioandaliwa na kituo cha runinga cha MTV Base kama sehemu ya kusherekea tuzo za MTV Africa mwaka huu iliyofanyika Mei 16,2014  kwenye Ukumbi wa Billcanas,jijini Dar es Salaam  Diamond alisema kuwa anafanya muziki wa Afrika na ndio maana amepata mafanikio makubwa. wasanii waliotumbuiza ni pamoja na Sauti Solo,Mi Casa Msic

Alisema kuwa wasanii wanatakiwa kujituma zaidi ili kuhakikisaha wanafikia malengo zaidi.

“Ninafanya muziki wenye ladha ya Afrika na hivyo ninatarajia kufanya vizuri zaidi katika tuzo za MTV nawaomba Watanzania wazidi kunipigia kura ili niweze kuibuka kinara, wasanii wanatakiwa kufanya juhudi za ziada kwa kutoa kazi nzuri ili kuhakikisha wanafikia malengo,” alisema

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 17, 2014

    Diamond muziki mzuri lakini vaa suruali yako kiunoni utaeshimiwa na utakua unawaeshimu wengine pia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...