Kwa muda mrefu tumekuwa tukicheza games zetu bila kutoa matokeo, hii imetokana na ukweli kwamba timu yetu iko kwenye kiwango cha juu sana hivyo timu pinzani zimekuwa zikichezea vichapo vya kuanzia goli 6 kwenda juu, hali iliyopelekea timu nyingi kugoma kucheza na Golden Bush Veterans ambao ndio mabingwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa kutambua hilo timu yetu imelazimika kucheza mechi na timu ambazo zinaweza kuleta upinzani kidogo huko mikoani na hapa jijini.

Ili kutekeleza program hiyo, kocha mkuu Madaraka Seleman ameanza game ya kukata na shoka na ndugu zetu wa Stakishali siku ya jumapili katika uwanja wa Kinesi. Game hiyo itakuwa na upinzani mkubwa sana kutokana na historia iliyojengeka kwa muda mrefu kwamba mechi  inayohusu timu hizi mbili imekuwa ya kukata na shoka.

Game hii itachezwa katika uwanja wa Kinesi kuanzia saa mbili kamili na mwamuzi atakuwa bwana Othman Kazi akisaidiwa na waamuzi wawili wa pembeni. Aidha Golden Bush tutatumia mechi hii kama maandalizi kabambe ya timu yetu itakayokuwa na safari ndefu kuelekea Mafinga na Makamboko kucheza game za kirafiki na veterans wa huko mwishoni mwa mwezi june.

Tunawakaribisha kwa kila hali mjue mshuhudie kikosi kilichosheheni vipaji kama vile Sadik Muhimbo, Said Kokoo, Said Swed, Salum Athuman, Herry Morris, Waziri Mahadhi, Nico Nyagawa, Omary Mgonja “Carzola”, Abuu Mtiro, Tom Morris na wengine wengi wakiongozwa na kocha Madaraka Selemani.

Asanteni kwa kunisikiliza.
Onesmo Waziri “Ticotico”
Msemaji na mchezaji mwandamizi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...