ZOEZI
la kupiga marufuku bodaboda na bajaji zinazofanya biashara katikati ya
Jiji la Dar es Salaam limegeuka biashara kwa Halmashauri ya Jiji la Dar
es Salaam hasa kwa watumiaji wa pikipiki hizo kwa ajili ya usafiri
binafsi wa kawaida kwenda na kurudi kazini, pamoja na makampuni
yanayotumia chombo hicho cha usafiri.
Halmashauri
ya jiji sasa imeanza kuwatoza watu binafsi na makampuni yanayotumia
chombo hicho shilingi 500 kwa siku kila bodaboda inapoingia mjini
wakidai ni tozo ya chombo hicho kupata idhini ya kuingia mjini kwa kila
siku.
Wakizungumza
na mtandao huu jana baadhi ya wananchi wamelalamikia kitendo cha
Halmashauri ya Jiji kugeuza zuio la kufanya biashara ya bodaboda
katikati ya jiji aina ya biashara ya kujipatia fedha kwa kutoza shilingi
mia tano kwa siku kwa kila pikipiki za watu binafsi na makampuni
zinapoingia mjini.
Mkazi
wa Jiji, Jackson Chalamila alisema tayari amelipia kibali cha miezi
sita yaani shilingi 90,000 kama tozo ya kuingia mjini kila siku na
ameruhusiwa kuingia mjini na pikipiki yake anayodai huitumia kama chombo
cha usafiri kwenda na kurudi kazini kila siku za kazi.
Baadhi
ya madereva wa pikipiki wanaozitumia kama vyombo vya usafiri binafsi
kwenda na kurudi kazini wakihoji juu ya mkanganyiko huo katika ofisi za
Jiji la Dar es Salaam, juzi. Hata hivyo hawakupata majibu zaidi ya
kukuta tangazo lililositisha upokeaji wa toza za kuingia mjini na
vibali.
"...Binafsi
nimelipia kutokana na usumbufu ambao ninaupata toka kwa mgambo wa jiji
kila siku wanatukamata ukiwaonesha kitambulisho cha kazi kinachokuonesha
kuwa wewe hufanyi biashara ya bodaboda hawakitambui na wanasema
unatakiwa kuwa na kibali, hivyo nikalazimika kukata baada ya kulipia
shilingi 90,000," alisema Chalamila.
Aliongeza
kuwa hata hivyo utaratibu huo si wa haki bali ni namna ya kuwanyonya
wananchi kwani mtu hawezi kulipishwa tozo za kuingia mjini kwa chombo
anachokitumia kama usafiri wake wa kwenda na kurudi kazini, ilhali
magari hayalipi tozo yoyote ya kuingia mjini.
Tangazo lililobandikwa na Jiji kusitisha zoezi la ukusanyaji wa tozo/vibali vya kuingia mjini na pikipiki.
"Huu
ni utapeli mtupu, sisi tunalipa kodi kama ilivyo kwa magari binafsi na
ni chombo cha moto mtu unakitumia kama usafiri wako iweje ulipishwe kila
siku unapoingia mjini? Mbona watu wanaotumia magari kama usafiri
binafsi hawalipi wanapoingia mjini? Huu ni wizi...," alisema.
Mwandishi
wa habari hizi alifika hadi ofisi ya Jiji kutaka kupata ufafanuzi juu
ya malalamiko hayo ya baadhi ya wafanyakazi wanaotumia pikipiki kwa
ajili ya shughuli zao binafsi na kutozwa ushuru wa kuingia mjini, lakini
haikufanikiwa kumpata msemaji wa jiji ambapo walizi walidai ametoka nje
ya ofisi kikazi.
Mwandishi
wa habari hii alishuhudia tangazo lililowekwa na Jiji la kuwarifu
wananchi kuwa limesitisha malipo ya tozo za pikipiki kuingia mjini hadi
hapo itakapotangazwa tena, ili kutoa nafasi kwa jiji kukagua vibali
vilivyotolewa na kuvihakiki kabla ya kuendelea. Hata hivyo baada ya
mkanganyiko huo baadhi ya watu waliolipia walianza kufika katika ofisi
hizo wakitaka kurejeshewa fedha zao na wengine kuhoji kadhia hiyo.
kesi ufunguliwe dhidi ya halmashauri. ni nnjia pekee ya kuuondoa dhulma. ifunguliwe hadi mahakama ya rufaa. gharama zote za kesi kama aliyefungua akishinda ilipe halmashauri na pia iwarudishie pesa zao wale wote waliokata kibali hicho
ReplyDeleteKwanza halmashauri ianze kuondoa magereji kwenye mitaa tunayoishi watu, ndio waanze bugudha nyingine kwa sisi watu tusio na sauti, tumepeleka malalamiko ya kuwekewa gereji jirani na nyumba zetu,hawaangalii kero tunazopata, kama harufu kali ya rangi, kelele za kunyoosha magari, leo hii wanaangalia usumbufu wa bajaji na pikipiki, kwa nini hamuangalii kero za wananchi kazi kuendekeza rushwa,
ReplyDeleteAskari mgambo na askari polisi imekuwa ni mradi kushika waendesha pikipiki na kutengeneza hela. Mara nyingi inatokea Askari mgambo anauliza mwendesha piki kuhusa kibali ya kuedeshea hapo hana sare maalum yeye binafsi kujitambulisha kama aonekane je yuko kazini, hawa askari mgambo je wanakuwa kweli kazini?
ReplyDelete