Mashabiki wa Mchezo wa soka nchini wakishangilia ushindi wa timu Timu ya Real Madrid iliyoshinda kwa magoli 4 -1 na kunyakua ubingwa wa UEFA kwa mwaka 2014/15 dhidi ya ndugu zao Atretoco Madrid katika fainali iliyofanyika mjini Lisbon,Ureno.Heineken Tanzania ilichukua nafasi hiyo kwa kuonyesha mechi hiyo kwa lengo la kuwakutanisha mashabiki wa soka hapa nchini,ambapo shughuli hiyo ya kuonyesha mchezo huo ilifanyika kwenye Hoteli ya Golden Tulip hotel,Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Heineken Tanzania,Uche Unigwe akiongea na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kuonyesha soka la fainali ya UEFA Champions Leage uliopigwa jana usiku mjini Lisbon,Ureno na kupatikana kwa Bingwa mpya msimu huu,Timu ya Real Madrid ya Hispania.
Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF),Jamal Malinzi nae likuwa ni mmoja wa waliohudhulia hafla hiyo na hapa akihojiwa na waandishi wa habri juu ya mchezo huo wa Fainali ya UEFA.
Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF),Jamal Malinzi akiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja wa Heineken Tanzania,Uche Unigwe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...