Spika wa Bunge kesho tarehe 26 Mei 2014 atakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Semina ya 25 ya Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola ambayo itafanyika hapa nchini kuanzia tarehe 25/05/2014 mpaka 31/05/2014.
emina hiyo ambayo ni mfululizo wa hatua za mafunzo na kubadilishana uzoefu kwa Wabunge wa nchi wanachama wa CPA itahudhuriwa na Wabunge zaidi ya 60 toka nchi 18 ambazo ni Australia, Ghana, Seychelles, Kenya Uganda na Nigeria.
Nchi nyingine ni pamoja na Sri Lanka, Bangladesh, Uingereza, Namibia, Pakistan (Khyber Panktunkwa), Kiribati , Trinidad & Tobago, Guyana, New Zealand na Scotland. Wajumbe wengine watatoka nchi za Zambia, Malaysia, Swaziland, Tasmania, Cook Island, Rajastan, New South Wales, Uttar Pradesh, Western Australia, Zanzibar, Tanzania, Chandigara, Australia Capital Territory, South Australia, Cook Islands, na India.
Mwenyekiti WA Sekretarieti ya Maandalizi ya Semina ya 25 ya CPA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa toka Ofisi ya Bunge, Ndg. Jossey Mwakasyuka akiongea na waandishi wa Habari kuhusu kuanza kwa semina hiyo. Kulia na Ndg. Elisa Mbise Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi na Ndg. Said Yakubu Mratibu wa CPA Kanda ya Tanzania. Picha na Owen Mwandumbya
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...