Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea maua muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ndjili jijini Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) usiku wa kuamkia leo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) Augustin Matata Ponyo Mapon akimkaribisha na kuzungumza na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili katika mji mkuu wan chi hiyo Kinshasa kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.Rais Kikwete baada ya atakutana na mwenyeji wake Rais Joseph Kabila na kufanya naye mazungumzo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali na kumpa pole balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) Mh.Anthony Ngereza Chehe aliyelazwa katika hospitali ya Ngaliema Health Centre jijnii Kinshasa baada ya kuugua malaria.Rais Kikwete yupo jijini Kinshasa DRC kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Picha na Freddy Maro
Kweli tembea ujionee, hiyo ndio hospitali ya kulazwa waheshimiwa Kongo?
ReplyDeleteSio hivyo mdau. ni kwa vile ni malaria tu, kama ingekuwa na zaidi ya malaria angelazwa yenye hadhi kama Hospitali ya Ilala hivi.
ReplyDeleteMdau wa kwanza ni nini hasa kilichokutisha? ni kitanda? au sakafu?? au ulipenda uone mi mitambo na minyaya nyaya kibao ndio ukubari???au labda jina la hospitali halianzi na swaga zile tulizozizoea za .....kwa mtazamo wa haraka haraka mwakilishi wetu hajambo huoni hata tabasamu????
ReplyDeleteMdau wa kwanza sijakuelewa. Mimi sioni tofauti na hospitali za bongo. Mgonjwa katibiwa ndiyo la muhimu. Tena angalao sakafu yao ina tiles za kwetu nyingi zina sakafu aliyoicha mkoloni.
ReplyDeleteHapo ni katika health center (kituo cha afya) na mhe. aliwekwa bed rest (mapumziko)huku akimalizia dose ya malaria, hakuwa amelazwa (admitted) katika hospitali kubwa. Hata hivyo mdau wa kwanza ulitarajia ukute sofa set katika zahanati!!!
ReplyDelete