Wakazi wa Kata ya Kizengi wakishangilia jambo,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akizungumza nao,mara baada ya kuweka jiwe la msingi na kuzindua Ofisi ya chama hicho.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa Kata ya Kizengi,Wilayani Uyui mkoani Tabora,wakati wa ziara yake iliyoendelea mkoani humo.Kinana amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kusikiliza kero mbalimbali za Wananchi ili kuchukua hatua na kuzishughulikia,aidha katika ziara hiyo Kinana pia ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye.
Ndugu Kinana amehutubia mamia ya wananchi kwenye mkutano hadhara uliofanyika katika Kata ya Loya,ambapo kuliibuka sintofahamu ya baadhi ya mambo ikiwemo Mbunge wa Jimbo Igalula, Mhandisi Athuman Mfutakamba kutokuwa na tabia ya kuwatembelea wananchi wake na kujua matatizo waliyonayo, hali iliyosababisha Wananchi wamzomee alipopanda jukwaani kuhutubia na kujibu maswali aliyoulizwa ambapo ilibidi Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kuingilia kati na kurejesha hali ya utulivu na kumtaka Mbunge wa jimbo hilo Mh,Athumani Mfutakamba kuwa na tabia ya kuwatembelea wananchi wake.
Aidha kauli hiyo imekuja,kufuatia Wananchi kulalamika wazi kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na kutokubali utendaji kazi wa Mbunge huyo.Wananchi hao waliweka wazi kuwa Mbunge huyo amekuwa akipiga porojo tu kwa mambo mengi ,badala ya kuwasikiliza na kutatua matatizo yanayowakabili amekuwa akiingia mitini.
Wananchi hao wakatolea mfano wa Zahanati ya Kata hiyo ambayo haina jokofu la kuhifadhia chanjo za watoto na Dawa,kwamba aliahidi kulishughulikia lakini hakuna utekelezaji uliofanyika hadi sasa,kama vile haitoshi Wananchi hao wakoangeza kuwa mara baada ya kuchaguliwa Mbunge huyo aliwaahidi kuwaletea mnara wa mawasiliano ya simu za mikononi kwa muda wa siku 100,ambalo ndio tatizo kubwa kwa kata hiyo ya Loya,lakini hakulitekeleza mpaka sasa.
Hata hivyo katika kuweka mambo sawa kwa Mbunge huyo,katibu Mkuu wa CCM,Ndugu kinana aliwaeleza wananchi kuwa atawasaidia kufuatilia suala hilo la mawasiliano,na pia amewaahidi kuwanunulia jokofu hilo kwa wananchi wa Kata ya Loya wilayani Uyui mkoani Tabora.
Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye,akiwahutubia wakazi wa Kata ya Kizengi waliojitokeza kwa wingi,Wilayani Uyui mkoani Tabora,kwenye mkutano wa hadhara.
Mbunge wa Jimbo la Igalura,Mh.Athuman Mfutakamba,akieleza maendeleo ya miradi mbalimbali iliyotekelezwa na chama cha CCM,kufuata Ilani ya chama hicho,katika kijiji cha Loya,Wilayani Uyui mkoni Tabora.
Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Uyui,Mussa Ntimizi akizungumza na Wananchi wa Kata ya Kizengi wakati akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi katika Ofisi ya chama hicho na kuzungumza na wananchi.
PICHA NA MICHUZIJR-UYUI-TABORA
ZAIDI BOFYA HAPA
PICHA NA MICHUZIJR-UYUI-TABORA
ZAIDI BOFYA HAPA
Nimependekeza kwenye katiba kiwepo kifungu cha kuwatathmini wabunge wanapofikia nusu ya muhula kusudi wakiboronga wasiruhusiwe kugombea muhula mwingine.
ReplyDelete