Kanali Dr. Edward Massala kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) akifuatilia majumuisho ya Mkutano wa Tatu wa Maadalizi ( Prep CoM) ya mapitio ya Mkataba wa Kimataifa wa Uzuiaji wa Usambaaji Holela wa Silaya za Nyukilia ( NPT) Mkutano huo wa maandalizi ulifanyikak wa wiki mbili hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Ingawa wajumbe kutoka nchi 149 kati ya 189 ambazo ni wanachama wa NPT hawakutoka na makubaliano ya pamoja kuhusu mapendekezo na mpango wa utekelezaji vinavyokusudiwa kuwasilishwa kwenye mkutano huo wamapitio utakaofanyika mwaka 2015. jambo la msingi ambalo kila nchi inalikubali ni kwamba hakuna nchi au shirika litakaloweza kukabiliana na madhara ya mlipuko wa silaha za nyukilia na kwamba jambo la muhimu ni kuondokana kabisa na silaha hizo ili dunia iwe mahali salama. Nyuma ya Kanali Massalla ni Bw. Abdalla Khamis, Afisa katika Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa

Na Mwandishi Maalum

Mkutano wa Tatu wa maandalizi ( Prep Com) ya mkutano utakaofanyia mapitio ya Mkataba wa Kimataifa Unaozuia Usambaaji Holela wa Silaha za Nyukilia ( NPT) umemalizika mwishoni mwa wiki iliyopita, huku wanachama wakitoka bila ya kuwa na makubaliano ya pamoja kuhusu mapendekezo na mpango wa utelelezaji yatakayowasilishwa katika mkutano huo wa mapitio unaotarajiwa kufanyika mwaka 2015.

Licha ya kwamba nchi hizo hazikutoka na makubaliano ya pamoja, jambo la msingi na ambalo linakubalika na wote ni kwamba hakuna nchi au shirika la kimataifa linatakaloweza kukabiliana na madhara ya mlipuko wa silaha za nyukilia iwe kwa makusudi au kwa bahati mbaya.

Na kwa sababu hiyo nchi 136 zilizochangia hoja ya madhara ya silaha za nyukilia kwa binadamu zilisisitiza kuwa njia pekee ya kumwepusha mwanadamu na madhara hayo ni kuondokana au kuachana kabisa na silaha za hizo.

Hata hivyo, nchi zinazomiliki silaha za nyukilia ambazo ni Ufaransa, Marekani, Uingereza, China na Urusi, licha ya kutambua madhara ya silaha hizo, zenyewe zimependekeza kuwa upunguzaji wa silaha hizo, ufanyike hatua kwa hatua.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa mkutano huo uliofanyika kwa wiki mbili kuanzia April 28 hadi Mei Tisa, Mwenyekiti wa mkutano huo wa Tatu Mwakilishi wa Kudumu wa Peru katika Umoja wa Mataifa, Balozi Enrique Roman – Morey alieleza kwamba kutofikiwa kwa makubaliano ya pamoja kuhusu mapendekezo na mpango wa utekelezaji hakukutokana na kutokuwepo wa utashi wa kisiasa baina ya wajumbe bali ni ufinyu wa muda zaidi wa majadiliano.

Kwa mujibu wa Balozi Morey nchi 149 kati ya 189 ambazo ni wanachama wa NPT walihudhuria mkutano huo. Na kwamba nchi tano zinazomiliki silaha za nyukilia yaani Marekani, Urusi, Uchina, Ufaransa na Marekani, ziliwasilisha taariza zao zinazofanana kuhusu mchakato unaoendelea wa kupunguza malimbikizo ya silaha hizo.

Mwenye kiti huyo wa Prep Com alibainsha kwamba nchi wa wanachama wa NPT walijadili vipengele muhimu vinayounda NPT ambavyo ni uzuiaji wa usambaaji holela wa silaha za nyukilia, upokonyaji wa silaha za nyukilia, matumizi salama ya nishati ya nyukilia, madhara ya nyukilia kwa mwanadamu na Uanzishwaji wa Ukanda huru dhidi ya silaha za nyukilia na silaha zingine za maangamizi katika eneo la Mashariki ya kati.

Aidha Balozi alieleza pia kwamba jambo jingine lililojadiliwa kwa mapana na wanachama wa NPT ni kuhusu haja na umuhimu wa mataifa kuridhia mkataba wa kimataifa unaozuia majaribio ya silaha za nyukilia (CTBT). Hadi sasa ni nchi 162 tu ndizo zilizoridhia mkataba huo.

Jambo la muhimu ambalo Mwenyekiti wa PrepCom anasema lilionekana dhahiri katika mkutano huo ni kuwa nchi zote zilizoshirikia mkutano huo wa maandalizi, zimeonyesha uwajibikaji katika kuhakikisha kuwa Dunia inaondoka na inakuwa huru dhidi ya silaha za nyukilia.

Mapendekezo na mpango wa utekelezaji uliopitishwa mwishoni mwa mkutano huo, utawasilishwa na Mwenyekiti wakati wa mkutano wa mapitio ya NPT utakofanyika mwezi Mei mwaka 2015.

Ujumbe wa Tanzania katika mkutao huo uliongozwa na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi akiwamo mtaalamu kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Kanali Dr. Edward Massala.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...