Katibu MKuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba,Mh.Yahaya Nawanda katika kijiji cha Kiselya,wilayani Iramba,mkoani Singida,pichani kati ni Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi,Mwigulu Nchemba.Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikad,siasa na Uenezi Nape Nnauye,wakiwa kwenye ziara ya Kukagua kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Chama,kukagua maandalizi ya uchaguzi ya serikali za mitaa,kusikiliza kero za wananchi na kuzitafututia ufumbuzi.
 . Katibu MKuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi,Mh.Mwigulu Nchemba mara baada ya kupokelewa katika kijiji cha Kiselya,Wilaya ya Iramba, mkoani Singida.
 Katibu wa NEC Itikad,siasa na Uenezi Nape Nnauye akizungumza jambo na Katibu wa NEC Itikadi,siasa na Uenezi Nape Nnauye mara baada ya kuwasili wilayani Iramba,na msafara mzima wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana ukitokea Wilayani Ikungi.Kinana yuko mkoani Singida kwa ziara ya siku nane.
 Ndugu Kinana akiwa sambamba na Wananchi wakishiriki kubeba mawe kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa Kituo cha Afya katika kijiji cha Kiselya Wilayani Iramba mkoani Singida iliyojengwa kwa nguvu za Wanchi.
Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi,Mh.Mwigulu Nchemba akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mbele ya Wananchi wa Kijiji cha Kiselya,wakati wa ushiriki wa ujenzi wa kituo cha afya cha Kiselya,wilayani Iramba mkoani Singida
 Wananchi wa kijiji cha Kiselya wakishangilia jambo,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozungumza nao,kwenye mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya kijijini hapo.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wajumbe wa kamati ya Siasa Wilaya,ambapo pia alisomewa Taarifa ya CCM wilaya  pamoja na taarifa ya utekekelezaji Ilani ya CCM .
PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZJR.BLOGSPOT.COM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mzee wangu kinan naomba kasi ulio anza nayo wala wa sikurudishe nyuma tangu urudi kuna mafanikio meme na unatutia hamasa sana na ukiwa mkweli kama unavyo waahidi wanachama wako na amini kabisa katika uchaguzi ujao majimbo mengi tunachukuwa,tunataka hilo jimbo la Lisu,Mdee,Mnyika,Sugun na mchungaji wake na kule Arusha majimbo yote yarudi ccm na matusi yao yatakoma.Juhudi zako ndio zitakazo fanya yote hayo.pole Kazi nzuri unayo ifanya Baba.Mungu akubariki sana

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 25, 2014

    Napelegwa naona yupo nyumbani. Karibu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...