Katibu Mkuu wa ICAO Bw. Raymond Benjamin akipata maelezo mafupi kutoka kwa Kaimu Meneja Huduma za Hali ya Hewa kwa Usafiri wa Anga Bw. John Mayunga alipotembelea Kituo cha Hali ya Hewa kilichopo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Katika ziara hiyo Bw Raymond alipendezewa na jinsi Mamlaka ilivyoboresha huduma kwa kutumia teknolojia ambapo wateja wanapata ‘flight Folders’ za taarifa za hali ya hewa kwa njia ya kielekronikali (Aviation Information System (AIS). Huduma hii ni moja ya maboresho yaliyofanywa na TMA katika kukidhi matakwa ya wateja wa usafiri wa anga kwa kuzingatia sera ya ubora (QMS) ya Mamlaka yenye kusisitiza uboreshaji wa huduma kulingana na mahitaji ya wakati husika. TMA ni moja ya taasisi za hali ya hewa chache na za awali kutunikiwa cheti cha ubora wa Kimataifa (ISO:9001:2008) katika ukanda wa nchi za Afrika na kuendelea kukidhi matakwa ya kukimiliki cheti hicho mpaka sasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...