Kiingilio cha chini cha mechi ya kirafiki kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Malawi (Flames) itakayofanyika Jumanne (Mei 27 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000.

Washabiki watakaolipa kiingilio hicho ni kwa wale watakaokaa kwenye viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani. Kwa upande wa VIP B na C kiingilio kitakuwa sh. 10,000 wakati kwa VIP A itakuwa ni sh. 20,000.

Mechi hiyo itaanza saa 11 kamili jioni ili kutoa fursa kwa washabiki wengi zaidi kuishuhudia kwa vile itakuwa ni siku ya kazi.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itawasili asubuhi ya siku hiyo hiyo ya mechi kutoka Tukuyu mkoani Mbeya ambapo imepiga kambi yake chini ya Kocha Mholanzi Mart Nooij.

Malawi (Flames) inayonolewa na mchezaji wake wa zamani Young Chidmozi tayari ipo nchini kwa ajili ya mechi hiyo inayotumiwa na timu zote kama maandalizi ya mwisho kwa ajili mechi za mchujo za Kombe la Afrika (AFCON).

Wakati Stars kwenye mechi za AFCON itarudiana na Zimbabwe jijini Harare, Flames nayo itakuwa ugenini N’djamena kukabili Chad.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO

SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...