Wadau wa bandari na reli wa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kampuni ya BESIX ya Ubelgiji baada ya kumaliza kikao cha pamoja na kampuni hiyo. Kampuni ya BESIX ilianzishwa mwaka 1909 na imeajiri watu 19,0000. Mwaka jana kampuni hiyo ilipata faida Euro 2.13 bilioni. Pamoja na mambo mengine, kampuni hiyo imehaidi kusaidia shughuli za jamii Tanzania kupitia taasisi yake inayosaidia shughuli mbalimbali za jamii (BESIX FOUNDATION).
Wadau wa reli na bandari wakishuhudia mtambo wa kuzalisha umeme unaotengenezwa na kampuni ya ABC ya Ubelgiji kwa ajili ya wilaya ya Biharamulo. Uongozi wa kampuni ya ABC ulieleza kwamba matengenezo ya mitambo ya kuzalisha umeme kwa ajili ya Biharamulo, Ngara na Mpanda unaendelea vizuri.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...