Katibu MKuu wa CCM,Ndugu Kinana akikata utepe kuashiria uzinduzi wa wakala wa uuzaji wa matrekta kwa wanavikundi,yanayouzwa na Vijana SACCOS LTD,ya Igunga,inayojumuisha vikundi mbalimbali vya wilaya hiyo,wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali pamoja na wananchi wilayani humo,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Igunga,Mh.Elibariki Kingu.
Ndugu Kinana akiwasha moja ya trekta mara baada ya kuuzindua uwakala wa zana za kilimo wa Vijana SACCOS LTD wilayani humo.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua shamba la alizeti la  ekali 25 la Kikundi cha Vijana katika Kijiji cha Iborogero, wilayani Igunga, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama , kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za Wananchi.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitazama mmea wa alizeti,wakati alipokwenda kagua shamba la alizeti la  ekali 25 la Kikundi cha Vijana katika Kijiji cha Iborogero, wilayani Igunga, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama , kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za Wananchi.
Sehemu ya shamba la alizeti la  ekali 25 la Kikundi cha Vijana katika Kijiji cha Iborogero, wilayani Igunga, wakati  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipokagua wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama , kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za Wananchi.
 Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akihututubia katika katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika  Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mjini Igunga, ambapo alisifu utenaji a Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Elibariki Kingu na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo pamoja na  Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kwa uchapakazi wao. pamoja na ubunifu wa miradi mbalimbali ya kuwasaida vijana.
  Baadhi ya Wafuasi wa chama cha CCM na Wananchi mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye uwanja wa Sokoine mjini Igunga jioni ya leo,kwenye mkutano wa hadhara ambapo Katibu Mkutano wa CCM,Ndugu Kinana alihutubia.
 Katibu wa Itikadi n Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika  Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mjini Igunga.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (pichani shoto) akimpokea aliyekuwa Katibu wa chama cha CUF Wilaya ya Igunga, Michael Maganga (aliyenyoosha kadi yake ya CUF juu), aliyeamua kukihama chama hicho na kujiunga na CCM katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa Sokoine.Kinana amemaliza leo ziara yake wilayani humo kuhamia wilaya ya Nzega hapo kesho kuendelea na ziara ya siku 10 mkoani Tabora.

PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 10, 2014

    AMA KWELI ALIZETI NI MMEA AMA ZAO LA CCM!

    Nadhani hicho cha ziada ndicho kilicho mvutia Mhe. A. Kinana.

    Angalieni rangi zake, maua ya rangi ya Njaro na Majani ya rangi ya Kijani!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...