![]() |
Wakurugenzi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakikagua moja ya Mradi unao tekelezwa na CDA) katika mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN). |
![]() |
Katibu Mkuu Ofisi ya waziri Mkuu Dkt : Florens M Turuka wa (katikati) akitoa maelekezo kwa Wakurugenzi wa OWM walipo tembelea eneo la mradi wa Makaburi ya Viongozi katika eneo la Mlimani . |
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (CDA) Bw: Pascal Muragiri akitoa maelezo ya mradi wa Barabara unaotekelezwa na CDA kwa msaada wa Benki ya Dunia wanao wakati wa Ziara ya Katibu Mkuu OWM Mkoani Dodoma
.............................. .............................. ..................
Akizungumza na Wakurugenzi wa Idara na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt: Florens M. Turuka amesema lengo la kutembelea miradi ni kujionea mwenywe yeye na Wakurugenzi na wakuu wa Taasisi ili kuweza kujiridhisha na mana ya uwendelezaji wa Miradi hiyo inayosimamiwa na Serikali.
Miongoni mwa miradi iliyo tenmbelewa ni Mradi wa Makaburi ya viongozi ambapo mradi huu uko katiaka hatua za Mwisho za kukamilisha kuwalipa fidia wakazi wa eneo husiaka ili kupisha mradi huo uendelee .
Aidha pamoja na mradi wa makaburi pia waliweza kutembelea miradi ya upimaji viwanja vya makazi na eneo la uwekezaji katiaka eneo la Njedengwa njekidogo ya Manispaa ya Dododm unao tekelezwa na Mamlaka ya Uastawishaji Makao Makuu Dododma (CDA)
Naye kaimu Mkurugengenzi wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Mkuu Dododma (CDA) Bw: Pascal Murugiri amesema mradi wa Njedengwa umegarimu jumla ya ya kiasi cha Shilingi Bilioni 15 ikiwa kama mkopo kutoka benki hivyo nifursa sasa kwa wananchi kuja (CDA) na kujipatia viwanja amabavyo viko tayari vikiwa na huduma zote za msingi kama Barabara za lami Umeme na Maji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...