HAYATI BALOZI WILSON TIBAIJUKA
 8 Januari 1945 - 20 Mei 2000

Ni miaka 14 sasa tangu ulipotuacha na kwenda mahala pema zaidi. Umekuwa katika nyoyo zetu na mawazo yetu wakati wote na maisha hayakuweza tena kuwa kama ilivyokuwa zamani.

Kuishi bila wewe tunafarijiwa na baraka za Mwenyezi Mungu na kumbukumbu nzuri kwa yale tuliyoshiriki pamoja sehemu mbali mbali duniani na upendo na staha uliotupa katika maisha yako yote. Unakumbukwa kwa upendo na wanafamilia wote wa ukoo mzima wa Tibaijuka, ndugu, jamaa, majirani na marafiki.

Kutokuwepo kwako kamwe si mwisho wa mapenzi yetu kwako bali mwanzo wake! Lala salama mpaka tutakapokutana tena katika maisha ya amani ya milele.

-Amina-

Kwa Uvumilivu Tutayashinda Yote

"Furahini siku zote, Ombeni bila kukoma, Shukuruni kwa kila
 jambo, maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo
Yesu. Wathesalonike (1) 5:16-23
.
Kutakuwepo na Ibada ya Misa ya ukumbusho wa Hayati Balozi Wilson Tibaijuka, leo tarehe 20 Mei, 2014 saa kumi na  moja jioni katika nyumba ya familia Makongo Juu, Jijini Dar es Salaam. Itafatiwa na kujumuika hadi saa nne usiku. Mnakaribishwa.

Maelekezo: Muga Tibaijuka (0786214141) au Kemi Tibaijuka (0783991244)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...